Header Ads Widget

BIMA HAITAKULINDA, TUSHIRIKI UCHAGUZI KWA AMANI DKT, SAADA MKUYA

 

Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima Medja Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema kuwa uchaguzi bila vurugu unawezekana, na ametoa wito kwa Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo muhimu kwa njia ya amani, utulivu na kuheshimu sheria za nchi.

Akizungumza jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Mkuya alisisitiza kuwa bima haiwezi kufidia madhara yanayotokana na machafuko au vurugu za kisiasa, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kulinda maisha yao, mali zao na mustakabali wa taifa kwa kuepuka migogoro na kuzingatia misingi ya demokrasia.


“Tushiriki uchaguzi kwa njia ya amani na utulivu tukivunja sheria, tukajeruhiwa au kupoteza mali zetu, bima haitaweza kutulinda katika hali hizo nijukumu letu kujiepusha na machafuko kwa manufaa yetu binafsi na ya taifa kwa ujumla,” alisema Dk, Mkuya.

Katika hafla hiyo, taarifa ya utendaji wa soko la bima kwa mwaka 2024 iliwasilishwa, ikionyesha ukuaji chanya wa sekta hiyo na mchango wake katika kukuza uchumi wa taifa. 

Waziri Mkuya alizitaka taasisi za bima kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuelewa umuhimu wa bima, huku akiwasisitiza kutumia huduma hizo kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI