Header Ads Widget

ZITTO AAHIDI MAENDELEO WANACHI WA PEMBEZONI WALIOTELEKEZWA


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MGOMBEA ubunge wa chama cha ACT Wazalendo katika jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe amesema kuwa utekelezaji duni wa mbinu ya maeneo ya pembezoni ya manispaa ya Kigoma Ujiji umesababisha hali duni za maisha ya wananchi wa maeneo hayo hivyo akiingia madarakani atatoa kipaumbele katika utekelezaji wa kupeleka maendeleo kwenye maeneo hayo.

akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za ubunge kwa ajili ya uchaguzi mkuu mkutano uliofanyika kwenye kata ya Businde manispaa ya Kigoma Ujiji Zitto alisema kuwa hali ya kuachwa nyuma kimaendeleo kwa maeneo hayo kumeleta tofauti kubwa ya maisha  baina ya wananchi wa maeneo hayo na wale wa kati kati ya manispaa.

Mgombea huyo alisema kuwa kutokuwepo kwa barabara za uhakika kuunganisha maeneo hayo na maeneo ya miji hivyo shughuli nyingi za kiuchumi zimedumaa na watu wengi hawataki kwenda kuwekeza huko kwa sababu ya changamoto hiyo ya miundo mbinu.


Alibainisha kuwa hata katika huduma za kijamii bado maeneo hayo yamekumbwa na changamoto ya uhaba mkubwa wa walimu ikiwemo shule ya Sekondari Businde yenye walimu sita ambapo  wazazi wanalazimika kuchanga shilingi 6000 ili kulipa walimu wa kujitolea.

Kuhusu suala la ardhi aliwataka wananchi wa maeneo hayo kupima maeneo yao na kushughulikia hati za ardhi ili ugawaji wa maeneo unaofanywa kwa wawekezaji usije kuwaathiri kwa kuporwa maeneo yao akiahidi pia kushughulikia wananchi waliotoa maeneo yao kwenye eneo la KISEZ na ujenzi wa uwanja wa ndege ambayo yamechukuliwa na serikali na hadi sasa hawajalipwa.

Akizungumza katika mkutano huo Mgombea udiwani wa kata ya Businde, Saidi Makala alisema kuwa watu wa eneo hilo wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuporwa maeneo yao bila fidia kwa sababu diwani aliyekuwepo alikuwa akishirikiana na serikali katika uporaji huo hivyo kuomba wananchi wamchague ili awasimamie kuhakikisha maeneo yao hayaporwi kwa kigezo cha uwekezaji.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI