Header Ads Widget

WANANCHI WA TANGA WAJIANDAA KUMPOKEA RAIS DKT. SAMIA

.NA AMINA SAIDI, TANGA 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwasili Mkoani Tanga mnamo Septemba28 ziara yake itaanza jioni katika eneo la mkata Wilayani Handeni Dkt Samia ambaye pia ni mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)anakuja kwa ajili ya ziara ya kikazina kisiasa katika mkoa huo.


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ostadhi Rajab Abdul Rahman alithibitisha ujio wa mgombea urais wa chama hicho ,Akizungumza na waandishi  wa habari alieleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwafikia l wananchi wote wa Tanga bila kujali itikadi zao za kisiasa ,aliitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi alisisitiza kwamba mgombea huyo ataleta maendeleo yatakayonufaisha wote. 


Aidha alisema kuwa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwasili Mkoani Tanga mnamo Septemba 28,Ziara yake itaanza jioni katika eneo la Mkata Wilayani Handeni Dkt .Samia ambaye pia ni mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)anakuja kwa ajili ya ziara ya kikazi na kisiasa katika mkoa huo. 


Aliongeza kusema kuwa Mh.Rais Dkt Samia  atakuwa na  ziara ya takribani siku tatu ndani ya mkoa wa Tanga ambapo atapita muheza na Korogwe ambapo ratiba itaendelea kutolewa ili wananchi wote wapate taarifa juu ya ujio huo.


"Sisi imani ni kwamba wananchi watakipigia Chama chetu na Daktari Samia suluhu Hassan kwani tumeona maendeleao makubwa kupitia uongozi wa Kiongozi wetu hivyo hakuna kiongozi yeyote ambaye yuko thabiti ambaye  ataleta maendeleo katika mkoa wetu kwaajili ya wananchi wote"alisema Rajabu.


Alisem kuwa kupitia Rais Samia wananchi waendelee kutegemea maendeleo zaidi kwani baada ya ziara yake kikazi aliyoifanya kwa miezi michache iliyopita  amefanya mabadiliko  katika kuhuakikisha miradi ambayo ilikuwa inasuasua sasa inadelea kwa kasi  zaidi.


Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Tanga wametoa maoni yao kuhusu ujio wa Mh.Rais Dkt Samia Suluhu na kusema wananahitaji kwanza kuona aje aone changamoto mbalimbali ikiwemo maisha ya mwananchi mmojommoja na barabara ya pangani pia aikazie mkazo mkubwa zaidi kwani kuna baadhi ya maeneo mvua ikinyesha kunapitika kwa taabu sana 


Ibrahim Saidi ni mmoja ya wananchi aliyetoa maoni alisema kuwa ujio wake kama Mgombea urais wa Chama Tawala amesema wao kama wananchi wanatarajia  kuona Dkt.Samia atatatua changamoto ya wananchi mbalimbali lakini pia awangalie na wanyabiashara wadogowadogo wapewe fursa mbalimbali kupitia ujio wake.


mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI