Ufaransa imetumbukia katika mzozo mpya wa kisiasa baada ya kushindwa kwa Waziri Mkuu François Bayrou katika kura ya imani katika Bunge la taifa.
Kushindwa kwa Bayrou kwa kura 364 dhidi ya 194 kunamaanisha kwamba Jumanne atawasilisha barua ya kujiuzulu kwa serikali yake kwa Rais Emmanuel Macron, ambaye lazima sasa aamue kuhusu hatua zitakazofuata. Ofisi ya Macron ilisema hii itafanyika "katika siku zijazo".
Hatua zitakazochukuliwa na kumtaja waziri mkuu mpya kutoka mrengo wa kulia wa kati; kuelekea kushoto na kutafuta jina linaloendana na Chama cha Kisoshalisti; na kuvunja bunge ili uchaguzi mpya ufanyike.
Bayrou amekuwa waziri mkuu wa kwanza katika historia ya Ufaransa ya miaka ya karibuni kuondolewa madarakani kwa kura ya imani badala ya kura ya kutokuwa na imani naye.
Ofisi ya rais wa Ufaransa ilisema katika taarifa yake kwamba rais Emmanuel Macron "amezingatia" matokeo na kusema atamtaja waziri mkuu mpya "katika siku zijazo", na kufikisha mwisho uvumi uliobaki kwamba rais badala yake anaweza kuitisha uchaguzi wa mapema.
Macron atakutana na Bayrou Jumanne "kukubali kujiuzulu kwa serikali yake", iliongeza.
Bayrou ni waziri mkuu wa sita chini ya Macron tangu kuchaguliwa kwake mnamo mwaka 2017 lakini wa tano tangu 2022. Kuondolewa kwa Bayrou kunamwacha mkuu huyo wa taifa la Ufaransa na mtihani mpya wa ndani ya nchi unaomumiza kichwa katika wakati anapoongoza juhudi za kidiplomasia kuhusu vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.
Maadui wakubwa wa Macron katika chama cha mrengo wa kushoto cha France Unbowed wanamtaka yeye binafsi kujiuzulu, lakini wachambuzi wachache wanafikiri hilo linawezekana.
Kwa hivyo Ufaransa iko njiani kupata waziri mkuu wa tano katika kipindi cha chini ya miaka miwili, rekodi mbaya ambayo inadhihirisha kuyumba na kutoridhika ambako kumetawala katika muhula wa pili wa rais nchini Ufaransa.
0 Comments