Israel imeanzisha mashambulizi ya anga Jumatatu jioni viungani mwa miji ya Homs na Latakia, nchini Syria, rasmi za vyombo vya habari vya Syria zimesema.
Uvamizi wa Israel ulilenga eneo la Maskana viungani mwa Homs.
Mashambulizi kama hayo ya ndege pia yalilenga maeneo ya karibu na eneo la Saqoubin nje kidogo ya Latakia, lakini hakuna hasara iliyoripotiwa, kulingana na shirika la habari la Syria, ambalo lilithibitisha kuwa magari ya zima moto yalitumwa kwenye eneo la shambulio hilo.
Kwa upande wake, Shirika la uangalizi wa haki za inadamu la Syria limeripoti kuwa "ndege za kivita za Israel zilifanya shambulizi la anga zikilenga kikosi cha anga kilichoko kusini mashariki mwa mji wa Homs. Milipuko mikubwa ilisikika katika eneo lililolengwa, huku kukiwa na ripoti za awali za uharibifu wa mali."
Wizara ya mambo ya nje ya Syria ililaani "uvamizi wa anga unaofanywa na vikosi vya Israel vinavyokalia kwa mabavu," kama ilivyoeleza, na kuyataka kama "ukiukaji wa wazi" wa sheria za kimataifa na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Ilisema kuwa uvamizi huu "ni sehemu ya mfululizo wa mashambulizi ya uchokozi yanayofanywa na Israeli kwenye ardhi ya Syria''.
0 Comments