Rais wa Marekani Donald Trump amesema hatairuhusu Israel kuuchukua ukingo wa Magharibi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House Rais Trump amesisitiza hilo halitafanyika.
Trump, ambaye anatarajiwa kukutana na Netanyahu Jumatatu ijayo, pia amesema mpango wa kukomesha mzozo wa Gaza "unakaribia" kufikiwa.
Israel inakabiliwa na ongezeko la shinikizo la kimataifa la kutaka kukomesha vita huko Gaza na kukalia kiabavu Ukingo wa Magharibi huku wimbi la mataifa ya Magharibi yakitambua rasmi taifa huru la Palestina.
Baadhi ya wanasiasa wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia wa serikali ya Israel wametaka Israel kutanua maeneo ya Palestina wanayoyakalia kimabavu baada ya Uingereza,Ufaransa na nchi nchi nyingine kutangaza kuitambua rasmi Palestina kama taifa.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kutoruhusu kuwepo kwa taifa huru la Palestina.
0 Comments