Aliyekuwa wa shirika la upelelezi la Marekani FBI James Comey ameshitakiwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwa Bunge la Marekani na kuzuia haki kutendeka.
Rais Trump alimfuta kazi Bwana Comey mnamo mwaka 2017,muda mfupi tu baada ya kuthibitika kuwa Rais huyo alikuwa anachunguzwa kuhusiana na madai kuwa Urusi iliingilia uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2016.
Mwanasheria Mkuu wa Marekani Pam Bondi alisema katika taarifa kwamba hati ya mashtaka "inaonyesha dhamira ya Idara hii ya Haki ya kuwawajibisha wale wanaotumia vibaya nyadhifa zao kuwapotosha Warekani".
Inaaminika kuwa mashitaka dhidi ya Comey yanahusiana na ushahidi alioutoa mbele ya kamati la Baraza la Seneti la masuala ya sheria ambapo alikanusha madai kuwa alifichua kwa vyombo vya habari taarifa nyeti kuhusu namna Urusi iliuingia uchaguzi wa Marekani.
Comey ni mkurugenzi wa kwanza wa zamani wa FBI kushtakiwa kwa uhalifu, ingawa anashikilia kuwa hajadanganya chini ya kiapo.
Ikiwa atapatikana na hatia, atakabiliwa na kifungwa cha hadi miaka mitano jela.
0 Comments