Header Ads Widget

TANAPA YAENDELEA KUPOKEA NYOMI LA WATALII, WATUMISHI WA SERIKALI WAFURIKA TARANGIRE


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linaendelea kunufaika na ongezeko la watalii wa ndani, ambapo safari za mafunzo na ziara za kitaaluma kwa viongozi na taasisi mbalimbali za umma zimezidi kushika kasi katika Hifadhi za Taifa.

Mwelekeo huo umeonekana wazi jana, Septemba 11, 2025, baada ya viongozi na watumishi wa Ofisi ya Mahakama Kuu, Mahakama ya Kazi, Mahakama ya Uchumi, Mahakama ya Ardhi, Wanasheria, Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya pamoja na Jeshi la Polisi kutembelea Hifadhi ya Taifa Tarangire. Wageni hao walipokelewa na Mkuu wa Kanda ya Kaskazini, Naibu Kamishna wa Uhifadhi Steria Ndaga pamoja na Mkuu wa Hifadhi hiyo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Beatrice Kessy.

Ziara hiyo ililenga kuhamasisha uelewa kuhusu uhifadhi, kujifunza zaidi kuhusu thamani ya rasilimali za Taifa, na kuchunguza fursa za uwekezaji zinazopatikana kupitia sekta ya utalii.

Ongezeko la ziara kama hizi linaonyesha mwamko mpya miongoni mwa wazawa, jambo linalosaidia kulinda urithi wa Taifa na kukuza mapato ya ndani kupitia utalii.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI