Header Ads Widget

DC CHUACHUA AWATAKA WANACHI KIGOMA KUMPOKEA SAMIA KWA UPENDO

 

                                    Mkuu wa wilaya Kigoma Dk.Rashid Chuachua

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mkuu wa wilaya Kigoma Dk.Rashid Chuachua amewataka wananchi wa mkoa Kigoma kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumuonyesha upendo Rais Samia Suluhu Hassan ambaye atafanya ziara ya siku mbili mkoani Kigoma kuanzia tarehe 13 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu huyo wa wilaya Kigoma alisema kuwa Rais Samia ataingia mkoani Kigoma Septemba 12 akitokea mkoani Tabora ambapo tarehe 13 Agosti atafanya mikutano katika wilaya za Uvinza, Kasulu na Buhigwe.

Sadiki Kadulo Katibu wa CCM wilaya Kigoma Mjini (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari

Dk.Chuachua alisema kuwa tarehe 14 Rais Samia atafanya mkutano mkubwa wa kampeni katika viwanja vya Katosho Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo aliwataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi kusikiliza sera, ilani na mambo ambayo serikali imeyafanya lakini pia ataeleza mipango ambayo serikali yake itafanya kwa miaka mitano ijayo.

Mkuu wa wilaya Kigoma Dk.Rashid Chuachua akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake

Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Kigomaa ,Sadiki Kadulo akizungumza na Waandishi wa habari ujio wa Rais Samia mkoani Kigoma alisema kuwa wanatarajia kufanya mkutano mkubwa ambao utavunja rekodi ya watu watakaohudhuria hivyo amewataka kuja kusikiliza mambo ambayo kiongozi huyo amekuja nayo.

Kadulo alisemaa kuwa Rais Samia amefanya makubwa makubwa katika miaka yake minne aliyokuwa Rais wa nchii na kwa mkoa Kigoma ipo miradi mingi na mikubwa ambayo imefanya hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kusikiliza mambo gani mapya ambayo kiongozi huyo amekuja nayo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI