Na. Mwandishi Wetu Lindi.
TAASISI ya Pamoja Tutashinda Tanzania (PATUTA) wameshiriki uzinduzi wa kampeni Majimbo ya Mchinga na Mtama Mkoani Lindi, katika kuunga mkono juhudi kubwa za maendeleo ya Majimbo hayo.
Wana PATUTA wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Dkt. Aiden Ndaombwa Septema 7, 2025 katika Kijiji cha Rutamba wameweza kushiriki uzinduzi wa kampeni Jimbo la Mchinga linalotetewa na Mbunge Salma Kikwete wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kasimu Majaliwa.
Katika shamrashamra za uzinduzi huo Wana PATUTA waliweza kuamsha shangwe jukwaani kwa nyimbo mbali mbali ikiwemo wimbo wao maalum pamoja na hamasa mbalimbali.
Mbali na Jimbo hilo la Mchinga, pia Wana PATUTA Septemba 8, wameweza shiriki uzinduzi wa kampeni katika Jimbo la Mtama linaloongozwa na Nape Moses Nauye katika Kijiji cha Chiuta ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika tukio hilo, Wana PATUTA wameweza kutoa burudani ya kipekee sambamba na hamasa mbalimbali katika viwanja hivyo vya uzinduzi huo.
Aidha Dkt. Aiden Ndaombwa amewashukuru wana PATUTA kwa umoja wao kushikamana kwa nyati zote, huku pia akiwataka Watanzania kuendelea kudumisha amani na utulivu.
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva akipokea tisheti maalum ya PATUTA katika uzinduzi wa kampeni Jimbo la Mchinga |
![]() |
Mgombea Ubunge Jimbo la Mchinga,Mkoani Lindi Mhe Salma Kikwete akipokea tisheti maalum ya PATUTA |
0 Comments