Header Ads Widget

PUTIN ASEMA AMEFIKIA 'MAELEWANO' NA TRUMP KUMALIZA VITA UKRAINE

 

Rais wa Urusi Vladimir Putin anasema alifikia "maelewano" na Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mpamgo wa kumaliza vita vya Ukraine, katika mkutano wao huko Alaska mwezi uliopita.

Lakini hakusema kama atakubali mazungumzo ya amani na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky yaliyosimamiwa na Trump, ambaye inaonekana alitoa Jumatatu kama tarehe ya mwisho ya jibu la Putin.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kilele nchini China, Putin aliendelea kutetea uamuzi wake wa kuivamia Ukraine, kwa mara nyingine tena akilaumu vita dhidi ya nchi za Magharibi.

Kufuatia mkutano wa Alaska, mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff alisema Putin amekubali kudhaminiwa usalama wa Ukraine kama sehemu ya uwezekano wa makubaliano ya amani ya siku zijazo, ingawa Moscow bado haijathibitisha hilo.

Putin alikuwa akizungumza mjini Tianjin katika mkutano wa kilele wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai, ambapo alikutana na Xi Jinping na Narendra Modi.

Aliwashukuru viongozi wa China na India kwa msaada wao na juhudi zao za "kuwezesha utatuzi wa mgogoro wa Ukraine".

China na India ndio wanunuzi wakubwa wa mafuta ghafi ya Urusi, na yamekuwa yakikosolewa na mataifa ya Magharibi kwa kuunga mkono uchumi wa Urusi ambao umeathiriwa na juhudi za vita.

Katika hotuba yake, Putin pia alisema kwamba "maelewano yaliyofikiwa" katika mkutano wake na Trump huko Alaska ni "Hatua, kuelekea njia ya amani nchini Ukraine".

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI