Header Ads Widget

NJALU ANADI ILANI YA CCM AKIWASISITIZA WANANCHI KUPIGA KURA.

MGOMBEA Ubunge jimbo la Itilima Njalu Daudi Silanga, akiwasili kwenye moja ya Mkutano ya kampeni kunadi sera za Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.


MGOMBEA Ubunge jimbo la Itilima Njalu Daudi Silanga amendelea kunadi sera za Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwataka wananchi wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025 kupiga kura.


Njalu amesema wananchi wanalo jukumu moja la kupiga kura kwa wingi ili serikali ya CCM iendeele kuwatumikia na kuwaletea Maendeleo katika nyanja mbalimbali na kuongeza kuwa endapo watachagua viongozi wa CCM watarahisisha utendaji na Uwajibikaji.


Akizungumza na wananchi wa kata za Chinamili, Sagata, Mwaswale, Nkuyu, Migato na Mhunze, Mgombea huyo amewaomba kupiga kura za kishindo kwa Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge (Njalu) na Madiwani wa CCM.


"Tupeni mitano tena ili tuendelee kuboresha na kuimarisha miradi ya Maendeleo, kila Kijiji kuna huduma ya Umeme, Elimu, Afya na Maji...Mpeni Dk. Samia na Mimi Mbunge wenu pamoja na Madiwani wa CCM ili tuendelee kuchapa kazi" ameeleza Njalu.


Mwisho.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI