Na. Mwandishi Wetu, Kigamboni.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji uliopo Kata ya Somangira Wilaya ya Kigamboni, Mhe. Yohana Luhemeja 'Maziku' amefanya tafrija fupi ya kumpongeza Binti yake Rita Yohana kwa kumaliza Elimu ya Msingi.
Tafrija hiyo fupi imfanyika nyumbani kwake, Mbwamaji mwishoni mwa wiki huku wageni mbalimbali wakijumuika pamoja ikiwemo majirani, ndugu, jamaa na marafiki.
Awali, Mama wa Ubatizo Leah Simon Mbeshi ameweza kutoa neno la shukrani kwa familia ya Yohana kumlea binti yao katika maadili pamoja kumpatia elimu.
 |
Rita Yohana akimlisha keki Mama yake Mzazi |
 |
Rita Yohana akimlisha keki Baba yake Mzazi, Mhe. Yohana Luhemeja 'Maziku' ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji Gezaulole. |
 |
Rita Yohana akimlisha keki Mama wa Ubatizo |
Nae Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Tawi la Gezaulole, Abdala Mtandu amewapongeza Wazazi wa Rita Yohana kwa hatua njema ya kumpa elimu binti yao huyo ikiwa ni sera nzuri na utekelezaji wa Ilani ya CCM katika elimu hapa nchini ya kuhakikisha watoto wanapata elimu.
Kwa upande wa Wazazi wa Rita Yohana, Mhe Yohana Luhemeja 'Maziku' amewashukuru watu wote waliojumuika katika tukio hilo.
 |
Baadhi ya wageni katika tafrija hiyo ya Rita Yohana |
 |
Wageni walikuwa wakiselebuka |
 |
Rita Yohana akiwa na mdogo wake katika tafrija ya kuhitimu elimu ya Msingi. |
 |
Rita Yohana akiwa katika picha ya pamoja na Walimu wake wa shule ya Awali. |
0 Comments