Mgombea mwenza wa urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM) balozi Dkt Emanuel Nchimbi ameomba wananchi wa Jimbo la Isman kumpa kura za kutosha Mgombea Urais Dkt Samia Suluhu Hassan na katika ubunge kumpa Wiliam Vangimembe Lukuvi na madiwani wa CCM .
Alisema Kazi zolizofanywa na Rais Dkt Samia kwa kushirikiana na mbunge Lukuvi katika jimbo la Isman ni kubwa na ili kazi hizo kuendelea kufanyika wananchi hawanabudi kukichagua chama cha mapinduzi .
Dkt Nchimbi alisema Lukuvi ni mwalimu wake kisiasa na mshauri wake na alimtabiria kuwa atafika mbali na leo anauona utabiri wake.
Hivyo alisema wana CCM hawakukosea kumchagua Lukuvi kuwa mgombea wao Ubunge kwani kazi hiyo anaifahamu na ataendelea kuwatumikia vema .
Kuhusu maendelea jimbo la Ismani alisema CCM kimejipanga kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo la Isimani mkoani Iringa ili kukuza uchumi wa jimbo hilo.
Dkt Emmanuel Nchimbi alipokuwa akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa kampeni jimbo la Ismani katika kata ya Itunundu leo.
Balozi Nchimbi amesema katika jimbo la Ismani wamejipanga kutekeleza ilani katika sekta ya afya kwa kuboresha Hospitali ya wilaya, ujenzi wa vituo vya afya pamoja na ujenzi wa zahanati.
akizungumzia sekta ya maji Balozi Dkt. Nchimbi amesema wamejipanga kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kuchimba visima virefu vya maji katika jimbo la isimani ikiwa ni pamoja na kuboresha mabwawa ili kuendeleza sekta ya kilimo na ufugaji.
kuwa katika sekta ya elimu wamejipanga kujenga shule mpya za sekondari, shule za msingi .
Kwa upande wa Lukuvi alipongeza kazi kubwa zilizofanywa na serikali ya wamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia katika jimbo la Ismani kuwa miradi mingi imetekelezwa ambayo ni ukombozi kwa wananchi .
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara lami ya Ruaha- Samora itagharimu Kiasi cha Tsh billioni 142.5.
Alisema hivi sasa wakandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo wapo barabarani na bahati mbaya wameanzia mwisho kuja mjini lakini utawaona na kazi inakwenda vizuri sana lakini huu ni mradi wa kielelezo kwani huu mradi unaunganisha mkoa mzima na hii hifadhi ni kubwa sana Tanzania ni Hifadhi ya pili kwa ukumbwa nchini na mradi huu wa ujenzi wa barabara unakwenda na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Nduli na hii ndio ilikuwa ndoto yangu mwaka 1995 nilipokuwa nikigombea ubunge kila mmoja anajua.
Lukuvi alisema jambo la pili kubwa kwa jimbo la Isiman kuwa wakati anaingia ubunge mwaka 1995 shule ya sekondari Tangu 1995 sekondari zilikuwa ni 15 zikizojengwa kwa kipindi cha miaka 25 ni 9 na zilizojengwa kipindi cha awamu ya sita chini ya Dkt Samia zilizojengwa kwa kipindi cha miaka 25 ni 9 na zilizojengwa awamu ya sita inayoongozwa nawe Dr.Samia S.Hassan*
"sisi leo tuna sekondari 15 lakini katika miaka 25 tumejenga shule 6 tumejenga maana yake sisi na wananchi serikali ilikuwa ndio ilikuwa inatuunga mkono leo miama minne yako mheshimiwa Rais Dkt Samia umejenga shule sita za serikali bila wananchi kutoa pesa sasa hata kwa uwiano wa hesabu za kawaida wa miaka 25 na minne utaona kazi kubwa uliyofanya"*
Kuwa hizo ni shule zote lakini tumechelewa sana kupata 'A' Level kwani kwa kipindi changu chote cha miaka 25 jimbo la Isman tulikuwa na A level nne lakini wewe hivi sasa kwa kipindi cha miaka minne umeongeza shule za A level nne kwa hadi sasa shule zipo nane kati ya hizo nne zimejengwa kwa kipindi cha miaka 25 na nne kwa kipindi cha miaka nne ya Dkt Samia madarakani .
Mheshimiwa pamoja na hizo shule lakini leo jimbo la Isman umeanzisha mapinduzi kwenye sera ya elimu tunataka kwenda kwenye elimu ya kujitegemea lakini deni hilo kwa jimbo la Isman umeshalipa kuna chuo cha VETA Pawaga jimbo la Isman ambacho vijana masikini wanachangia kiasi cha Tsh 150,000 tu wanapata kitanda ,chakula na kila kitu kwa Tsh 150,000.
Aidha Lukuvi alisema kw upande wa vituo vya afya katika miaka 25 yote jimbo la Isman halijawahi kujengewa hata kimoja sio kwamba havipo vilikuwepo vinne kwa miaka yote 25 ila Zamani tulikuwa tunachukua Zahanati hivi na kugeuza kituo cha afya halafu tunaongeza wodi mbili na sisi kati ya vituo hivyo kimoja alikuja Marehemu Makamu wa Rais Dkt Omary akakizindua lakini ilikuwa Zahanati kituo cha faya hivyo kwa miaka 25 kulikuwa na Zahanati nne zilizopandishwa hadhi na kuwa vituo vya afya lakini miaka minne hii ya kwako vituo vilivyojengwa toka kwenye msingi vinne vipo jimbo la Isman vimeanza kutumika lakini kipo kimoja cha Ilolompya na Mahuninga pesa zipo huko huko milioni 800 za kukamilisha ujenzi huo .
Lakini baadae vituo vipya vya Migoli ,Isman na hospitali ya wilaya na kuletewa gari za wagonjwa mwaka jana kwa hiyo unaweza kujua kuwa hawa wananchi wa Isman wanafuraha kiasi gani kwa kazi kubwa walizofanyiwa na serikali hii ya awamu ya sita kwani huduma za afya bora zaidi na madaktari wapo mfano hapo Isman leo kuna madaktari kutoka huku Duniani walikuja kufanya kambi ya macho watu 8000 wamepata huduma pale kwa sababu kuna mashine ya upasuaji na hivyo hata wagonjwa kuja mjini kutibiwa kwa sasa hawafiki kabisa .
Pia alisema hata Hospital ya wilaya iliyojengwa na serikali ya awamu ya sita ipo jimbo la Isiman Pawaga pia alisema kuhusu huduma ya maji wananchi wa tarafa ya Isman toka nchi ipate Uhuru hawajawahi kuwa na huduma ya maji ya bomba na kwa kipindi chake chote cha ubunge amekuwa akibadili kila aina ya msamiati kuhusu kero ya maji lakini leo maji yanatoka Isman yote tena maji ya bomba safi na salama .
" kwa kuwa Ismani hakuna chanzo cha maji wewe uliagiza maji yavutwe kutoka Iringa mjini na mengine kutoka Kilolo na mradi huo umetekelezwa maji wananchi wanapata tena vijiji vyote kiasi cha Tsh Bilioni 9 zimetumika kusogeza huduma ya maji na sasa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Iringa (IRUWASA) ambayo ndio inatekeleza mradi huo uimeomba Tsh bilioni 3 ili kukamilisha kusogeza huduma ya maji kwenye vitongoji pia mheshimiwa Rais haya ninayoyasema naomba sana watu wa Isman wawe wanakuangalia sana wewe maana kila wakati wamekuwa wakisema wanakuombea sasa leo umekuja mwenyewe"
Hata hivyo Lukuvi alisema ukiacha tarafa mbili ya Isman ,tarafa mbili zimebalikiwa sana maana zinazungukwa na mto Ruaha ambao unamwaga maji yake bwawa la Mtera lakini maji hayo yamekuwa hayatumiki kwa uzalishaji ila sasa baada ya kipindi cha miaka minne ya Dkt Samia mto huo umekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wake.
Kuwa kwa kipindi chake Dkt Samia ameleta pesa kwa ajili ya liomba ujenzi wa mradi mkubwa wa umwagiliaji Pawaga Unaitwa Mkombozi wenye Bilioni 59.9 na kama haitoshi ameongeza pesa kiasi cha Tsh Bilioni 33.8 kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji wa Magozi miradi itakayoongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na miundo mbinu ya barabara kwa Pawaga kuwa na sehemu ya lami kidogo ikimpendeza japo haipo kwenye ilani basi kufikiliwa kuwa na wilaya ama Halmashauri yao wenyewe .
Pia alisema kwa wananchi wa Ismani kutokana na ukame wanaomba kama inawezekana kupata mabwawa ya umwagiliaji ili yaweze kutumika kipindi cha kiingazi kwa ajili ya shughuli za uzalishaji hivyo alisema kwa kuwa kipindi hicho ni cha kampeni za uchaguzi kwa niaba ya wananchi wa Isman wanahidi kutiki kura zote za ndio kwa mgombea Urais wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan kura ambazo mgombea mwingine yeyote hajawahi kupata ,Mbunge wa CCM na madiwani wote wa CCM Oktoba 29mwaka huu.
0 Comments