![]() |
Polisi Kata Somangira Wilaya ya Kigamboni, Samuel Ogudi akitoa Elimu kuhusu Usalama na Ulinzi Shirikishi kwa Mtaa wa Mbwamaji |
Na. Mwandishi Wetu, Kigamboni.
SERIKALI ya Mtaa wa Mbwamaji uliopo Kata ya Somangira Wilaya ya Kigamboni, imekutana na Wananchi wake katika kuweka sawa masuala ya Ulinzi na Usalama wa Mtaa huo ambao kwa pamoja wameridhia kuweka ulinzi Shirikishi kwa maendeleo ya Mtaa.
Awali, akitoa Elimu kwa Wananchi hao, Polisi Kata Somangira, Samuel Ogudi Amesema Wananchi wanajukumu la kuunda na kupanga masuala ya Ulinzi katika mitaa yao. Katika kikao hicho cha tatu cha kikanuni kwa Serikali za Mitaa, Wananchi kwa kauli moja wamekubaliana kuimalisha ulinzi shirikishi ndani ya mtaa huo ikiwemo kila mjumbe wa nyumba 10 awe na Makamanda wasiyo pungua watu (3), kila Kaya itachangia TSH 1,000 kwa ajili ya ulinzi. |
Yohana Luhemeja 'Maziku' ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Amesema:
"Kila mjumbe wa Serikali ya mtaa atapangiwa eneo lake la kusimamia ulinzi na usafi wa mazingira ataongozana na mjumbe wa nyumba 10 na makamanda wa ulinzi shirikishi, lengo mtaa wetu uwe safi na salama.
Aidha, Mwenyekiti amesema kuwa, watafanya kikao na wadau kwa ajili ya kusaidia kwenye suala zima la ulinzi.
"Ndugu Wananchi mikutano hii ndiyo ya kunikosoa na kuni sema kama kuna sehemu nimekosea.
Hata hivyo, Wajumbe walisema Mwenyekiti toka ameingia madarakani kuna mabadiliko makubwa sana amefanya ikiwemo:
Ukarabati ofisi ya Serikali ya Mtaa, Amefungua barabara ikiwemo kuweka vifusi kuziba mashimo makubwa.
Lakini pia amewapatia wanawake semina ya ujasiliamali wa utengenezaji wa bidha mbali mbali mfano sabuni ya maji, mabatiki, sabuni za vipande na mengine mengi.
Pia ameweza kuvuta maji na umeme kwenye jengo la ofisi ya Serikali ya Mtaa.
Mwenyekiti anapambana kila saa kuomba miradi mbali mbali kwa faida ya wananchi hakuna la kukukosoa bali tunakupongeza" wamesema Wananchi wa Mtaa huo wa Mbwamaji.
![]() |
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji,Mhe Yohana Luhemeja 'Maziku' akizungumza katika mkutano huo |
0 Comments