NA WILLIUM PAUL, SAME.
MGOMBEA Ubunge wa Chama cha Mapinduzi kupitia Jimbo la Same mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Anna Kilango Malecel ameahidi endapo atachakuguliwa atahakikisha kipindi cha miaka mitano barabara ya Mkomazi Same yenye urefu wa zaidi ya kilomita 100 inajengwa kwa kiwango cha lami.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika kata ya Maore ambapo alisema kuwa kipindi cha Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Sami Suluhu Hassan Jimbo hilo limepata fedha nyingi zaidi miradi ya maendeleo.
Alisema kwa awamu ya kwanza mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo kutokea Mkomazi hadi Ndungu ulishasainiwa na ujenzi ulishaanza hivyo atakapochaguliwa tena atahakikisha kipande kilichobaki kutokea Maore mpaka Same kinakamilika.
Alisema kuwa, asilimia 72 ya Tangawizi inayotumika hapa nchini huzalishwa katika jimbo la Same Mashariki ambapo aliitumia kama hoja muhimu ya kuomba ujenzi wa barabara ya Same Mkomazi kwa kiwango cha lami.
Kilango alidai kuwa Serikali imekubali kujenga barabara hiyo na kuahidi kuendelea kuisemea ambapo itasaidia kubadilisha uchumi kwa wananchi.
"Mkandarasi wa awamu ya kwanza ameshaanza na anajenga kilomita 36 kutoka Mkomazi mpaka Ndungu na Serikali imetenga zaidi ya Bilioni 59 kama Rais ameidhinisha fedha zote hizi tunaachaje kumpa kura zetu" alisema Anna Kilango.
Alisema kuwa, endapo watamchagua jambo la kwanza ataanza nalo akiingia Bungeni ni kuhakikisha Mkandarasi aliyepo Mroyo anarudi kazini kwa ajili ya ujenzi wa barabara kilomita 5, ili apambane kupata awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hiyo kutoka Maore mpaka Same kilomita 56 na mpaka sasa Mkandarasi ameshapatikana.
Alisema kuwa, kama kunamradi mgumu ni ya kujenga barabara kwa kiwango cha lami ambapo inamuhitaji Mbunge mzoefu mwenye sauti kali na kusimama imara na kuahidi atapambana kuhakikisha barabara hiyo inakamilika.
"Niwashukuru Wanachama wa CCM na Halmashauri kuu ya Taifa kwa kupendekeza jina langu kuwa mgombea, wanaccm na Wanachama wa vyama vya upinzani nawanyenyekea tumpe kura za kishindo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan maana kwa kipindi chake cha miaka minne amefanya mambo makubwa katika Jimbo letu" Alisema Anna Kilango.
Na kuongeza "Wakati Rais Samia anaingia madarakani Jimbo letu lilikuwa na kituo cha afya kimoja lakini kwa muda aliokaa madarakani ametujengea vituo vya afya vinne na kuboresha huduma katika kituo cha Afya Ndungu muone kwa kiasi gani kipindi cha miaka minne yake unaweza kumpaje kura za hapana anayekupenda mpende".
Katika sekta ya Elimu, Mgombea huyo alisema kuwa Rais Dkt Samia ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya Elimu ikiwemo ujenzi wa shule mpya za msingi na sekondari.
0 Comments