Header Ads Widget

KATIMBA AONYA UCHAGUZI USIVURUGE UNDUGU WA WATANZANIA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Naibu Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Zainab Katimba amewataka Watanzania kutokubali kupoteza Amani yao na kufarakanishwa na tofauti ya itikadi inayojitokeza wakati wa uchaguzi kwani chaguzi ni mambo ya muda na yanapita bali mahusino yao ni muhimu kama Watanzania.


 


Katimba ametoa kauli hiyo alipokuwa Mgeni Rasmi katika maulid ya kuzaliwa Mtume yaliyoandaliwa na Msikiti wa Muumin Ujiji mjini Kigoma na kutaka watanzania wote kufanya michakato ya uchaguzi kwa Amani na salama bila kugombana.


Naibu Waziri huyo wa TAMISEMI alisema kuwa serikali imeweka sheria na taratibu za uchaguzi ambazo kila Mtanzania anapaswa kuzifuata wakiwemo wagombea, viongozi wa vyama na wananchi wa kawaida hivyo kila mmoja anapaswa kufanya uchaguzi wa kistaarbu na kusimama kwenye nafasi yake bila jazba na kufanya maamuzi.

Sambamba na hilo Naibu Waziri Katimba aliwasihi waumin wa kiislam kusimamia mafundisho ya dini ya watoto wao kwani dini ndiyo msingi mkubwa wa kumfanya mwanadamu kuishi katika maisha ya kumcha Mungu na kufanya maovu ambayo hayaendani na misingi ya dini.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa Kigoma,Hassan Rugwa  amewasihi waumini wa kiislam mkoani Kigoma kuzingatia sana suala la Amani wakati huu ambapo nchi inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Raisi, Wabunge na madiwani kwa watu wote kufanya siasa za kistaarabu ambazo hazitavuruga Amani na usalama uliopo.

Akizungumza katika Sherehe hizo za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhamas (SAW) Kadhi wa mkoa Kigoma,AbdulMuhsin Kitumba alisema kuwa maulid hiyo ni siku tukufu kwa waislam katika kuenzi na kukumbuka mambo mema na mazuri yaliyofanywa na kiongozi huyo wa waislam ambayo hawana budi kuyaishi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI