Na Matukio Daima Media
HUKU kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu zikiendelea na chama cha mapinduzi (CCM) kabla ya kuanza kampeni zake kilifungua dirisha la wadau na wanachama wake kuchangia kampeni hizo kupitia harambee iliyokwisha fanyika ili kufanikisha safari hiyo Mainési Yoeli Kiwelu ameibuka na kutoa mchango wa wimbo wa kampeni.
Mchango huu unaleta taswira ya kipekee ndani ya CCM na jamii kuiga jambo hili jema kwa kila mmoja kuchangia anachoweza kufanikisha jambo kubwa la ushindi wa CCM.
Kama ilivyo nenwa na wahenga umoja ni nguvu hivyo ndivyo katika kampeni hizi kila mmoja ana mchango wake kujenga chama .
Kwani hata wale wanaotenga muda wa kufika kusikiliza sera mbali ya kuwa ni sehemu ya Demokrasia ila ni mchango mkubwa kwa chama na kumtia moyo na kumpa nguvu mgombea hasa anapokuta watu wengi wamejitokeza.
Mainesi Yoeli Kiwelu yeye amekuja na mchango huu wa wimbo zaidi ya mbili za kampeni za mgombea urais wa CCM Dkt Samia nyimbo ambazo zinaakisi kazi kubwa aliyoifanya .
Nyimbo hizo ni pamoja na CCM namba moja na Samia Tunakwenda nae oktoba tunatiki nyimbo ambazo ukizisikiliza hazichoshi bali zinakuvutia kuendelea kusikiliza tena na tena na mbali ya kuburudisha zinakumbusha kazi nzuri zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita na zile zinazokusudiwa kufanyika awamu ya saba.
Mainesi Yoeli Kiwelu si jina geni hasa ndani ya wilaya ya Mufindi pia mkoa wa Iringa na sasa Tanzania ni jina linalojulikana katika siasa, sanaa na uongozi wa wanawake mkoani Iringa na Tanzania kwa ujumla.
Mainesi ni kiongozi mstaafu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Mufindi kwa nafasi ya uenyekiti ambaye safari yake ya kisiasa na kijamii imejaa mafanikio na historia ya kuigwa.
Mbali na siasa, Mainési pia ni mwimbaji wa nyimbo mbalimbali za kizalendo, kidini na kisiasa, akiweka alama ya kipekee kwa kutoa zawadi ya wimbo wa kampeni kwa mgombea urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutokana na kazi kubwa aliyofanya katika uongozi wake wa awamu ya sita.
Maines katika mahojiano yake na Matukio Daima Media anasema kuwa shauku yake ni kuwatumikia wanawake na jamii kwa ujumla ndio maana alianza kama Katibu wa UWT Kata ya Wambi katika wilaya ya Mufindi Mji wa Mafinga.
Hapo ndipo alipothibitisha uwezo wake wa kuunganisha wanachama, kusimamia shughuli za chama na kuhamasisha mshikamano miongoni mwa wanawake.
Uchapakazi wake na imani aliyopewa na wanachama ulimpelekea kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mufindi, nafasi aliyoibuka mshindi na kuongoza kwa mafanikio makubwa.
Kutokana na mchango wake mkubwa, Mainési hakubaki katika nafasi moja tu.
Aliendelea kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama na taasisi zake za wanawake.
Hivi sasa, licha ya kustaafu nafasi ya Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mufindi, bado anaendelea kushiriki kikamilifu katika uongozi kwani ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Wilaya ya Mufindi kupitia nafasi moja ya uwakilishi wa UWT kwenda Halmashauri ya Wilaya, ambapo anatoa maoni na mawazo yenye kujenga katika sera na utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya wanawake.
Aidha, Mainési ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Mufindi, chombo muhimu kinachoratibu na kusimamia utekelezaji wa sera za CCM katika ngazi ya wilaya.
Hii inadhihirisha jinsi anavyoendelea kuwa sauti ya wanawake na jamii katika masuala ya kisiasa na kijamii.
Mbali na majukumu yake ya wilaya, Mainési pia amepata heshima kubwa ya kuwa Katibu wa Wanawake na Samia Mkoa wa Iringa nfasi hii inamhusisha moja kwa moja na kampeni na mikakati ya kuhakikisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaungwa mkono ipasavyo na wanawake mkoani humo.
kwani anasimamia na kuratibu harakati za wanawake wanaomuunga mkono Rais Samia, kuhakikisha mafanikio ya kisiasa na maendeleo yanaendelezwa.
Sanaa kama Nyenzo ya Uhamasishaji
Tofauti na viongozi wengi wa kisiasa, Mainési Yoeli Kiwelu ameweza kutumia kipaji chake cha muziki kama jukwaa la kuhamasisha jamii.
Ameimba nyimbo nyingi zikiwemo za Chama Cha Mapinduzi (CCM), nyimbo za Serikali na pia nyimbo za dini.
Muziki wake umebeba ujumbe wa mshikamano, mshikikiano na mshangao wa maendeleo yaliyofanikishwa na chama na serikali.
Kipengele cha kipekee kinachomtambulisha zaidi ni hatua yake ya kipekee ya kutoa zawadi ya wimbo wa kampeni kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Wimbo huu unakuja kama heshima kwa kazi kubwa aliyoifanya Rais Samia katika kipindi chake cha uongozi wa awamu ya sita.
kwani ni kazi inayodhihirisha namna anavyothamini mafanikio ya serikali na dhamira yake ya kuona CCM inaendelea kushika hatamu za uongozi nchini.
Uongozi na Maendeleo ya Wanawake
Katika kipindi chake akiwa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mufindi, Mainési alijipambanua kwa kupigania maendeleo ya wanawake, hususan maeneo ya vijijini. Aliwahamasisha wanawake kushiriki katika miradi ya kiuchumi, vikundi vya ujasiriamali na kujiunga na SACCOS ili kupata mikopo midogo midogo.
Ni wazi kupitia jitihada zake, wanawake wengi waliweza kujikwamua kiuchumi na kuwa sehemu ya maendeleo ya familia zao.
Vilevile, Mainési amekuwa mstari wa mbele katika kampeni za elimu ya mtoto wa kike, akihimiza wazazi na jamii kwa ujumla kuwapa watoto wa kike nafasi sawa ya kupata elimu bora.
Mainesi amejikita pia katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, akitumia nafasi yake katika UWT kuelimisha jamii juu ya madhara ya vitendo hivyo na umuhimu wa mshikamano wa kijamii.
Mchango katika CCM na Taifa
MainĂ©si Kiwelu anaamini katika misingi ya chama chake – umoja, mshikamano na maendeleo ya watu.
Kupitia uongozi wake na muziki wake, amechangia pakubwa katika kuimarisha taswira ya CCM ndani ya Mufindi na mkoa mzima wa Iringa.
Wimbo wake wa kampeni kwa Rais Samia unakuwa ni mfano halisi wa mchango wake binafsi kwa chama na serikali, ukiakisi mshikamano na mshikikiano wa wanachama wa CCM na viongozi wao.
Kumheshimu Rais Samia Suluhu Hassan
Kwa Mainési, Rais Samia ni kielelezo cha uthubutu, hekima na uongozi wa mfano anamwona kama shujaa wa wanawake, aliyevunja vikwazo na kuonyesha dunia kwamba mwanamke anaweza kuongoza taifa kubwa kwa busara na maono ya mbali.
Kupitia kazi kubwa ya Rais Samia katika nyanja za uchumi, elimu, afya, miundombinu na diplomasia ya kimataifa, Mainési amehamasika kutoa zawadi yake ya muziki kama njia ya kumshukuru na kumpongeza kwa uongozi wake thabiti.
Mainési Yoeli Kiwelu ni kielelezo cha mwanamke shujaa ambaye ameweza kuchanganya siasa, uongozi na sanaa kwa mafanikio makubwa.
Ikumbukwe kuwa Mainesi ni kiongozi aliyeanza safari yake katika ngazi ya kata na kufika kwenye majukwaa ya mkoa, huku akibaki na moyo wa kuwatumikia wanawake na taifa kwa ujumla.
Hivyo kupitia muziki wake, ametoa mchango wa kipekee katika kampeni na harakati za chama, huku akithibitisha kuwa sanaa ni nyenzo madhubuti ya kuhamasisha maendeleo na mshikamano wa kisiasa.
Kupitia zawadi yake ya wimbo wa kampeni kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Mainési ameandika historia ya pekee itakayobaki katika kumbukumbu za siasa na muziki wa kizalendo nchini Tanzania. Ni mfano wa kuigwa kwa wanawake na vijana wote wanaotamani kuchangia maendeleo ya taifa kupitia nyanja mbalimbali.
Mainesi kwa nafasi yake ya katibu wa wanawake na Samia mkoa wa Iringa anasema anampongeza sana Rais Dkt Samia kwa kuwawezesha wanawake kuanzisha biashara ya kuuza mkaa rafiki na mazingira chini ya taasisi ya mwanamke na Samia ambayo iliasisiwa na Rosemary Senyamle mkuu wa mkoa wa Dodoma .
Pia Maines alimshukuru sana Rais Dkt Samia ambae kwa sasa ni mgombea Urais wa CCM kwa kuwainua wanawake kwa kuwalipia wanawake kwenda kusoma chuo cha ufundi Stadi Tanzania (VETA) na wengi wao wamepata mafunzo hayo chini ya ufadhili wake kupitia taasisi ya Wanawake na Samia ndio maana Ahsante yao wanawake wote ni Oktoba kutiki ili kupata kura za kimbunga kwa Rais Dkt Samia na CCM .
0 Comments