Header Ads Widget

JERY AZINDUA KAMPENI JIMBO LA UKONGA, AAHIDI MAMBO MAKUBWA

 

Na Fatma Ally Matukio Daima 

Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga Jery Silaa, amesema kutokana na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha  Mapinduzi (CCM) kwa mwaka 2020/2025 ulivyotekelezwa na Chama hicho hana shaka,  wananchi watarajie mambo makubwa endapo watakipa tena ridhaa Chama hicho kuongoza nchi.

Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Ukonga katika uzinduzi wa kampeni wa kijimbo amesema Serikali ya awamu ya sita kupitia ilani ya Chama hicho imetekeleza miradi mikubwa ya maendeleo hivyo wanakila sababu ya kukiombea kura nyingi za ndio katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu.

Akizungumzia mikakati yake akiingia madarakani kubadilisha Jimbo la Ukonga kuwa la kisasa kwa kujenga masoko ya kisasa Gongolamboto ,Zingiziwa,Chanika ili kuwapangia utaratibu wajasiriamali katika fursa za kiuchumi waweze kukuza uchumi wa nchi yao.

Katika hatua nyengine amewataka wagombea udiwani wa jimbo la Ukonga wakichaguliwa na wananchi wakaanze kazi ya kusimamia miradi ya maendeleo vizuri ambayo Rais Dkt.Samia aemelekeza  fedha pamoja na mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri ili kila mwanachi aweze kupata mikopo hiyo.

"Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati nikiwa mbunge wa jimbo la ukonga kabla kugawa kata 13 mpaka kubaki kata saba awali Jimbo la Ukonga lilinizidi ukubwa chupu chupu liniue lakini kwa sasa nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuligawa jimbo hii"amesema Jerry 

Aidha Jery amewataka wagombea udiwani saba wa Jimbo hilo kuwa mstari wa mbele kuwasaidia wananchi na kutekeleza ilani ya Chama hicho kama walivyoahidi wananchi.

Jerry amesema katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi alivyosimamia wakati uliopita Kata ya Pugu Bangulo sekta ya maji tanki kubwa Rais amefunga maji kwa sasa maji hayo yanalisha Pugu Bangulo,Gongolamboto,Kitunda,mpaka jimbo la Kivule ni kazi kubwa ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa fedha kufunga tanki kubwa la maji  kuwatua ndoo kichwani kina mama aliomba wananchi wa jimbo hilo kumpa zawadi Dkt.Samia kura zote za Urais .

Aidha amesema mengine aliyotekeleza utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi akiwa Meya wa Manispaa ya Ilala na Mbunge wa Jimbo la Ukonga ameweza kujenga hospitali ya Mama na Mtoto nguvu kazi Chanika ,ameweza kujenga Kituo cha afya Zingiziwa, Buyuni, Mvuti, Pugu Station, Mzinga Kituo cha afya golofa mbili Shilingi bilioni 9 zilitumika ,Mikongeni Kituo cha afya Gongolamboto na Jengo la Macho katika Hospitali ya Wilaya kivule  


Akizungumzia Sekta elimu amesema Dkt samia suluhu Hassan tangu aingie madarakani hakuna mzazi anatozwa pesa za ada, shule za kisasa zimejengwa Nyeburu,Kigezi chini, Yongwe, na shule za Sekondari Ukonga ya golofa mbili, Nguvu mpya, Zogoali, Gulukwa kwalala, Barabara njia sita Mwendokasi Gongolamboto Kariakoo Mpaka posta huku, Nishati ya umeme  inapatikana kwa asilimia 100 kwa wananchi wote.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Said Sidde amesema mpaka sasa CCM Wilaya ya Ilala kata nane wamepita bila kupingwa wanasubiri kupigiwa kura za ndio au hapana kwa wagombea wa kata hizo.

Mgombea ubunge Jimbo la Kivule Wilayani Ojambi Masaburi aliwataka wananchi wa jimbo la ukonga kumchagua Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Madiwani wa Ukonga pamoja na Jery Silaa, sababu amefanya mambo makubwa akiwa Wizara ya Ardhi na maendeleo ya makazi na sasa ni Waziri wa Habari na Mawasiliano



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI