Header Ads Widget

DKT,NCHIMBI ANATARAJIA KUWASILI KAGERA SEPTEMBA 6 MWAKA HUU.

Na Shemsa Mussa -Matukio Daima 

Kagera.

Mgombea mwenza wa Urais kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwasili mkoani Kagera Septemba sita mwaka huu kwa ziara ya siku mbili,ili kunadi sera,Ilani ya 2020-2035 na kuomba kura kwa wananchi.

Dk.Nchimbi akiwa mkoani humo atafanya mikutano ya adhala na kuhutubia wananchi katika maeneo mbalimbali akiwanadi wagombea wa ubunge na madiwani wanaotokana na chama hicho.

Katibu wa siasa,uenezi na mafunzo mkoani hapa Amim Mahmud  alisema Dk.Nchimbi atapokelewa Wilayani Biharamulo katika eneo la Nyakanazi ambapo atahutubia wananchi kwa kunadi sera,asubuhi ya Septemba saba atakwenda jimbo la Ngara na kuongea na wananchi katika mkutano wa adhara.


"Septemba saba hiyohiyo saa tano asubuhi atafanya mkutano katika jimbo la Kyerwa katika mji mdogo wa Nkwenda,kisha saa saba mchana atahutubia wanachi wa jimbo la Bukoba Vijijini na saa tisa jioni atanadi sera na wagombea katika jimbo la Bukoba Mjini eneo la viwanja vya shule ya msingi Kashai ambapo atahitimisha ziara yake "alieleza Mahmud 

Aidha aliomba wananchi wote kujitokeze kwa wingi kumpokea mgombea  mwenza na kusikiliza Sera za CCM


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI