Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Muliro Jumanne Muliro, amewakabidhi bendera ya Taifa askari wa kike wanaokwenda kushiriki mafunzo ya shirikisho la askari wa kike duniani (IAWP) nchini Scotland kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camillus Wambura.
Akizungumza katika hafla hiyo, Muliro amesema IGP Wambura anathamini mchango wa shirikisho hilo ambalo limekuwa kichocheo cha mabadiliko ya kiutendaji ndani ya Jeshi la Polisi tangu mafunzo hayo yaanze kufanyika katika nchi mbalimbali.
“Cha kwanza anawapongeza sana nyinyi ambao mnakwenda kushiriki katika mkutano huo na amesisitiza kuwa mkienda katika mkutano huo mkajifunze na anatarajia makubwa kutoka kwenu kutokana na mafunzo hayo na anatamani aone manufaaa ya nyinyi kwenda katika mkutano huo na aone matokeo makubwa mkienda huko”.
0 Comments