VUNJO.
MGOMBEA Mwenza wa chama cha Mapinduzi, Dkt Emmanuel Nchimbi amemnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, Enock Koola na kuwataka wananchi kumpa kura nyingi za kishindo.
Dkt. Nchimbi yupo katika ziara ya kampeni za kuomba kura mkoani Kilimanjaro ambapo leo amewahutubia wananchi wa Jimbo la Hai, Siha, Vunjo na Moshi mjini ambapo amewaomba wananchi kuwachagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa CCM ili waendelee kuwaletea maendeleo.
0 Comments