NA MATUKIO DAIMA MEDIA ZANZIBAR
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameweka wazi mikakati yake ya kudhibiti mfumko wa bei za vyakula kwa kuja na mpango wa kuweka maghala maalum yaliyofanywa kuhifadhia bidhaa za vyakula ili kutoa unafuu kwa wnanachi
Amesema mikakati yake ni kuandaa akiba ya chakula katika maghala kwa kununua bidhaa muhimu kama mchele pamoja na mafuta katkma msimu wa mavuno na kuyahifadhi katika maghala hayo ili kuyauza kwa bei ya kawaida pale bidhaa hizo zinapopatikana kwa gharama kubwa
Kuhusu hali ya uchumi amesema uchumi wa Zanzibar umekua kwa asilimia 7.4 kutoka asilimia 4 iliyokua mwaka 2020
0 Comments