Dkt Samia Suluhu Hassan mgombea Urais wa CCM
katibu wa wanawake na Samia mkoa wa Iringa Mainesi Kiwelu (Kulia) akimpongeza mmoja kati ya wanawake walionufaika na mafunzo ya Samia ,kulia kwake ni mwenyekiti wa wanawake na Samia mkoa wa Iringa Lediana Mafulu anayefuata mkuu wa wilaya ya Iringa Benjamin Sitta
Na Matukio Daima Media, Iringa
Katibu wa Umoja wa Wanawake na Samia Mkoa wa Iringa, Mainési Yoeli Kiwelu, amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuwainua wanawake kiuchumi kupitia mafunzo mbalimbali ya ufundi na fursa za kimaendeleo.
Akizungumza na matukio Daima Media , Kiwelu alisema kuwa wanawake wa mkoa huo sasa wameondokana na hali ya utegemezi baada ya kufaidika na mafunzo ya ufundi stadi yaliyoratibiwa kupitia Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) na kugharamiwa moja kwa moja na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia.
Mafunzo ya ufundi yaliyoleta tabasamu
Kwa mujibu wa Kiwelu, mafunzo hayo yamekuwa na tija kubwa kwani wanawake wengi waliokuwa wakikosa kipato cha kujiendeleza sasa wamepata ujuzi wa fani mbalimbali kama ushonaji, useremala, ufundi umeme, mapishi, pamoja na stadi nyingine za maisha.
Anasema hali hii imewapa wanawake Iringa nyuso za tabasamu kubwa, hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, kwa kuwa sasa wana nafasi ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya familia zao na jamii kwa ujumla.
Katibu wa Wanawake na Samia Mkoa wa Iringa Mainesi Kiwelu katikati akiwa na Wahitimu wa mafunzo VETA ya kupiga Rangi,tunampongeza sana Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kutupa Fursa ya Wanawake kusoma Veta Bure kukuza Vipaji vyetu“Wanawake wengi wa Iringa walikuwa wakitegemea msaada kutoka kwa waume zao au ndugu, lakini sasa kupitia mafunzo haya ya VETA tumekuwa na uwezo wa kujitegemea. Rais Samia ametufanya tuwe na sauti na nguvu ya kiuchumi. Hii ni zawadi kubwa kwetu wanawake,” alisema Kiwelu.
Fursa ya mkaa mbadala: Rafiki Briquettes
Pamoja na mafunzo ya ufundi, Katibu huyo wa wanawake alieleza kuwa Rais Samia amewawezesha pia kupata fursa ya kuuza mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes. Bidhaa hiyo imetambulishwa kama njia mbadala ya kupunguza ukataji wa miti na kulinda mazingira, huku ikiwapatia wanawake ajira na kipato cha uhakika.
Kiwelu alitumia nafasi hiyo kumshukuru kwa dhati Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt Venance Mwasse, maarufu kama Mjomba, kwa kushirikiana kwa karibu na wanawake wa Iringa na kutoa msaada wa kitaalamu pamoja na miundombinu ya kuendeleza mradi huo.
mkurugenzi Stanico Dkt Venance MwasseAlibainisha kuwa mkaa wa Rafiki Briquettes una faida nyingi kwa jamii, ikiwemo kupunguza gharama za matumizi ya nishati majumbani, kutunza mazingira kwa kupunguza ukataji miti, na kuongeza ajira kwa wanawake na vijana.
Ubunifu wa mavazi ya kampeni
Kwa upande wake binafsi, Mainési Kiwelu alifafanua kuwa kupitia mafunzo hayo amebuni njia mpya ya kimaisha kwa kuanzisha ubunifu wa mavazi maalum ya kampeni za Rais Dkt. Samia na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Anasema vazi hizo zinauzwa kwa gharama nafuu na zimepokelewa vizuri na wananchi, hali inayoonyesha kuwa wanawake wamepata fursa ya kuchangia siasa na uchumi kwa wakati mmoja.
“Ubunifu huu umeniongezea kipato na kunifanya nione kwamba kweli wanawake tukipewa nafasi tunaweza kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa letu,” aliongeza Kiwelu kwa furaha.
Sababu za wanawake kuunga mkono Samia
Kiwelu alitaja sababu kuu zinazowafanya wanawake wa mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kuendelea kuwa na furaha na kumuunga mkono Rais Dkt. Samia katika uchaguzi ujao wa Oktoba 29. Alisema kuwa Rais amekuwa mstari wa mbele katika kuanzisha na kusimamia miradi mbalimbali inayowalenga wanawake moja kwa moja, ikiwemo miradi ya mikopo, mafunzo ya ujasiriamali, upatikanaji wa mitaji, na uwezeshaji wa masoko.
Aidha, miradi mikubwa ya kitaifa kama vile ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya na barabara, imewafaidi pia wanawake kwa kuwaondolea changamoto walizokuwa wakipitia kila siku. Kwa mfano, huduma bora za afya vijijini zimewapunguzia kina mama adha ya kutembea umbali mrefu kufuata matibabu.
Onyo kwa wanasiasa wa chuki
Sambamba na shukrani hizo, Kiwelu aliwataka wanawake na wananchi wote kupuuza wanasiasa wanaoeneza chuki na kupandikiza mbegu za mgawanyiko miongoni mwa Watanzania. Alisema kuwa ni muhimu kila mmoja kutambua kwamba amani na mshikamano wa taifa ni msingi wa maendeleo, na kwamba porojo zisizo na tija haziwezi kufanikisha maisha bora ya wananchi.
“Tukubali ukweli kwamba Rais wetu Dkt. Samia ana mapenzi ya dhati kwa wanawake na Watanzania kwa ujumla. Ameonyesha nia, uwezo na uthubutu katika kutekeleza miradi ya maendeleo. Hivyo wananchi wote tunapaswa kumuunga mkono kwa vitendo,” alisema kwa msisitizo.
Wito wa mshikamano
Kwa kumalizia, Katibu huyo wa wanawake na Samia mkoa wa Iringa alitoa wito kwa wanawake wote kuungana kwa mshikamano, kushirikiana kwa dhati, na kuendelea kutumia fursa zilizotolewa na serikali ya Rais Dkt. Samia ili kuondokana na umasikini na utegemezi.
Alisisitiza kuwa kwa kuwa na mshikamano na mshikikano wa kijinsia, wanawake wanaweza kuwa chachu ya maendeleo endelevu na kushiriki kikamilifu katika siasa, uchumi, na jamii.
“Wanawake wa Iringa tuna sababu ya kutabasamu, tuna sababu ya kushukuru na tuna sababu ya kuendelea kumuunga mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan. yeye ndiye kioo cha matumaini mapya kwa wanawake na Watanzania wote,” alisema MainĂ©si Kiwelu huku akishangiliwa na wanawake wenzake.
0 Comments