Rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro, amehukumiwa kifungo cha miaka 27 na miezi mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kupanga mapinduzi ya kijeshi.
Jopo la majaji watano wa Mahakama ya juu lilitoa hukumu hiyo saa chache baada ya kumpata na hatia kiongozi huyo wa zamani.
Walisema ana hatia ya kuongoza njama iliyolenga kumuweka madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi wa 2022 na mpinzani wake wa mrengo wa kushoto, Luiz Inácio Lula da Silva.
Jopo la Mahakama ya Juu pia lilimzuia kuwania wadhifa wa umma hadi 2033.
Bolsonaro, ambaye aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani baada ya kutajwa kuwa ana hatari ya kukimbia, hakuhudhuria awamu hii ya mwisho ya kesi ana kwa ana.
Lakini siku za nyuma alisema ilibuniwa kumzuia kugombea katika uchaguzi wa urais wa 2026 - ingawa tayari alikuwa amezuiliwa kuongoza ofisi ya umma kwa mashtaka tofauti. Pia ameiita kesi hiyo "uonevu".
Maneno yake hapo awali yameungwa mkono na Rais wa Merika, Donald Trump, ambaye aliweka ushuru wa 50% kwa bidhaa za Brazil, kama kulipiza kisasi kwa mashtaka dhidi ya Bolsonaro.
0 Comments