Header Ads Widget

CHALAMILA ATUMA SALAMU ZA POLE KIFO CHA FRANK NYALUSI

 


Baada ya taarifa za Kifo cha aliyekuwa mwemyekiti wa Chadema jimbo la Iringa mjini Frank John Nyalusi ,mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ametuma salamu za pole kwa familia na wana Iringa kwa kifo hicho.


kupitia kundi maarufu ya Iringa Daima ambalo Chalamila ni mmoja wa wanakundi ameandika.

Ndg zangu wana Iringa Polen sana sana kwa Kuondokewa na na Ndg Frank Nyalusi, amekua kaka, na mtani wetu kisiasa, alikua mtu mwema na aliyependa kusimamia anachoamini.


Ni moja ya waliowahi kuwa Madiwan wenye misimamo thabiti Tuomboleze kwa sala na dua za kupokelewa mbinguni.

 Tujifunze yale mema aliyoyasimamia. Raha ya milele umpe  Ee Bwana, na mwana wa milele umwangazie, apumzike kwa amani ya Kristo

Amen

Hata hivyo katibu wa Chadema mkoa wa Iringa Leonard Kurujila amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Nyalusi na kuwa taarifa zaidi za mazishi zitatolewa leo 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI