Header Ads Widget

ZANZIBAR KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA SABA WA VIONGOZI WA DUNIA WA MIJI SALAMA


Jiji la Zanzibar limechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa unaohusisha Wastahiki Meyaa wa majiji mbalimbali duniani. 

Mkutano huo unatarajiwa kuwaleta pamoja zaidi ya wajumbe 150 kutoka nchi zaidi ya ishirini, wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya kiserikali, taasisi za elimu na utafiti, sekta binafsi, asasi za kiraia pamoja na mitandao ya kimataifa inayojikita katika kuimarisha usalama wa wanawake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar  Mahmoud Mussa amesema,  mkutano huo wa siku tatu unaoanza tarehe 26 katika hoteli ya Madinat El Bahri, utakuwa fursa muhimu ya kujifunza mambo mbalimbali pamoja na kuitangaza Zanzibar kimataifa.


Amesema mada zitakazojadiliwa zitahusisha mitazamo ya ndani ya jamii, kitaifa na kimataifa katika suala la kuendeleza miji salama, hatua ambayo itasaidia Zanzibar kuboresha mbinu zake za usalama wa wananchi, hususan wanawake na wasichana.

Kwa mujibu wa Mstahiki Meya, mkutano huu unaendana na mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhakikisha kila mwanamke na msichana anatembea mitaani bila hofu, anasoma shuleni, anafanya biashara masokoni na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jiji la Zanzibar.

Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Hussein Ali Mwinyi.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI