Header Ads Widget

YANGA SC YAIFUATA RAYON SPORT KIMATAIFA

 

Na leonard Johnson

Klabu ya wananchi Yanga sc yatua katika nchi ya Rwanda kwaajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa,Wananchi wanatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji wao Rayon Sports ya nchini Rwanda,Mechi hiyo itapigwa Ijumaa ya Agosti 15, saa 1:00 usiku.

Mchezo huo ni maalumu kwa timu ya Rayon sport kwasababu ni siku maalumu ya timu hiyo kuweza kutambulisha wachezaji wake wapya walio sajiliwa pamoja na Benchi la ufuindi,kwaajili ya maandalizi msimu mpya wa 2025/2026.

hivyo klabu ya Rayon sport imetoa mualiko kwa timu ya yanga sc kwani wana amini yanga sc ni kipimo sahihi cha kujipima ubora wao kuelekea msimu mpya wa mashindano ,hivyo wamesha fanya sajili zao na kukamilika ni muda wa kupima ujazo wa sajili walizo fanya .

kwa upande wa yanga sc wao bado hawajakamilisha usajili kuelekea msimu mpya wa mashindano ingawa kwa asilimia kadhaaa wamesha sajili wachezaji muhimu katika timu yao , hasa katika safu ya ushambuliaji ambapo wamejalibu kuziba mapengo yalio achwa nawachezaji wao muhimu walio ondoka kikosini msimu huu kama Khalid aucho,ambaye nafasi yake itachukuliwa na Balla Konte ,na Stephanie Azizi ki iliyo chukuliwa na Mohamed Doumbia,

kwa taarifa kamili ni kwamba tayari klabu ipo kigali Rwanda kwaajili ya mualiko huo wa kirafiki walio upata kutoka katika klabu hiyo ya Rayon sport .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI