Header Ads Widget

CHAN 2024: MARUFUKU KUINGIA VIWANJANI NA VIFAA HIVI CHAN-CAF

Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) limepiga marufuku watu kuingia viwanjani na vifaa vyenye viashiria vya kisiasa, dini au vile vinavyokinzana na wadhamini rasmi wa mashindano ya timu za za Taifa kwa wachezaji wa ligi za ndani ya nchi.

Afisa wa ulinzi na usalama wa kitaifa wa fainali hizo za Afrika kutoka Tanzania, Mratibu wa Polisi (SP) Hashim Abdallah amewataka mashabiki wa soka na watanzania kwa ujumla wanapoingia uwanjani kutazama mechi za fainali hizo kutoingia na nguo au vifaa vingine kama bendera zenye maandishi au alama zenye viashiria vya kiasiasa, dini, au hata vinavyo kinzana na wadhamini rasmi wa mashindano husika.

“Mtu yeyote anayevaa T-shirt ambayo inakinzana na wadhamini wa CAF, mfano ana jezi imeandikwa matangazo yoyote jezi za kidini viashiria vya kisiasa na kidini na mambo mengine hawataruhusiwa uwanjani watavuliwa hizo nguo, na watakwenda kubadilisha au kuigeuza ili mradi lile tangazo lisiweze kuonekana”

Siku za hivi karibuni Tanzania ilipigwa faini ya dola za kimarekani 10,000 kutokana na vitendo vya uvunjifu wa usalama kama ilivyoanishwa kwenye kifungu cha 82 na 83 cha kanuni za usalama za CAF.

Kanuni za FIFA zinakataza watu kuangia uwanjani na vifaa vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani. Hii si kwa mashabiki tu hata wachezaji wakati mwingine hupigwa faini kwa kuingia na vitu hivyo au kujichora maandishi kwenye nguo zao ambayo yanakinzana na kanuni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI