Na Mwandishi Wetu, Matukio Daima Media Kibaha
WATIA nia ya Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani waliokuwa Wabunge wamefanikiwa kuongoza kwenye kura za maoni huku wawili wakishindwa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo David Mramba alisema kuwa matokeo hayo ni ya majimbo 9 ya uchaguzi ya Mkoa huo.
Mramba alisema kuwa Jimbo la Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Ridhiwani Kikwete hakuwa na mpinzani ambapo alipigiwa kura za ndiyo 12,074 kati ya kura 12,245 na hapana kura 171.
Jimbo la Mkuranga aliyeongoza ni aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Abdala Ulega aliyepata kura 8,490 akifuatiwa na Mohamed Kilalile aliyepata kura 4,293, Gift Mipiko kura 440, Mwasiti Matola kura 180 na Prisca Ngweshemi.
Jimbo la Kisarawe aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Dk Seleman Jaffo ameongoza kwa kupata kura 4,412, Msafiri Mpendu kura 804, Salum Chaurembo 321, Haji Janguo kura 164 na Tabia Karega kura 117.
Jimbo la Mafia aliyeshinda ni Omary Kipanga aliongoza kwa kupata kura 1,186, Mbaraka Dau alipata kura 759, Omary Kimbau alipata kura 614 na Amina Tuki alipata kura 9.
Kwenye Jimbo la Bagamoyo aliyeongoza ni Subira Mgalu aliyepata kura 3,544 na kumshinda aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mharami Mkenge aliyepata kura 1,574.
Christina Henry alipata kura 133, Haji Ngwira alipata kura 47 na Mathiasi Kambi, Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa aliongoza kwa kupata kura 8,465, Salma Ponga alipata kura 34 na Seleman Mlekela kura 26.
Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa aliongoza kwa kura 3,247 na kumshinda aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Michael Mwakamo aliyepata kura 1,802, Eliachahofu alipata kura 176.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 2,824 Koka aliwashinda wagombea wengine watano ambapo alifuatiwa na Mussa Mansour aliyepata kura 1,775 na Abubakar Alawi aliyepata kura 727.
Wengine ni Dk Charles Mwamwaja aliyepata kura 282 akifuatiwa na Magreth Mwihava aliyepata kura 39 na Ibrahim Mkwiru aliyepata kura 35.
0 Comments