Na Shemsa Mussa -Matukio Daima
KAGERA.
Serikali imetoka ufadhili wa masomo ya elimu ya chuo kikuu kwa wahitimu wanne Wa kidato cha sita mwaka 2025 Katika Shule ya kemebos,huku Mkurugenzi Wa Shule hiyo akitoka kitita cha fedha Kwa Kila Mmoja.
Mkurugenzi wa shule za kaizirege na kemebos Bw Yusto Kaizirege amesema aliweza kuanzisha utowaji wa tuzo hizo ili kufanya hasama kwa wanafunzi wote ambao wafanya vizuri masomo yao ya kidato cha sita
Amesema licha ya Serikali kuwapa ufadhili huo Wa masomo pia uongozi wa shule umetoa tuzo kwa kila mshindi kwa kutoa kiasi cha sh.milioni tano Kwa Kila ili kuweka motisha kwa wanafunzi.
Aidha ameeleza kuwa hatojali Kwa idadi ya wanafunzi watakaokuwa wamefanya vizuri kwani tayari ameshaweka ahadi ya kutoa zawadi na kwamba atakuwa amerudisha ada ya mwaka Moja kwa mwanafunzi wa kidato cha sita.
Nae Mkuu wa shule hizo za kaizirege na kemebos Ndg Kisha Ilamulira amesema katika ufadhili huo shule hiyo imefanikiwa kupata wanafunzi watatu ambao wamepata udhali kutoka Serikalini ikiwa wawili watasoma vyuo vya ndani na mmoja ataenda kusoma nje ya nchi.
Amesema shule ilitumia muda kuwaandaa wanafunzi hasa wa mchepuo wa sayansi ambapo kwa mwaka 2025 Shule imefanikiwa kupata wanafunzi wanne wenye ushindi wa alama 3
"Anitha Sosthenes ambaye amepata alama tatu na kupata ufaulu wa juu atagarimiwa na Serikali kwenda kusoma nje ya nchi kwa kupata ufadhili wa Rais Wa nchi na hawa Christopher wambura na Cleophace wambura pamoja na Bright Gladson wataghalamiwa masomo Kwa kusoma ndani ya nchi"amesema Ilamulira
Mwl kisha,Amewataja Wahitimu hao ni Anitha Sosthenes Mchepuo Wa (PCM),Bright Gladson mchepuo wa (PCB), Christopher Wambura Chacha Mchepuo Wa (PCB) na Cleophace Wambura Chacha Kwa Mchepuo Wa (PCB)
Wote wakiwa na ufahulu Wa Division 1.3 kutoka shule binafsi ya sekondari Kemebos iliyopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.
Akielezea jinsi walivyoweza kufanikisha alama hizo Christopher wambura amesema ufaulu huo ni ushirikiano kati ya walimu waliokuwa wakifundisha shuleni .
Amesema, mbali na kufundishwa waliweza kutumia muda mwingi katika masomo na kujipa malengo ya kupata ufaulu wa juu zaidi na kuonyesha unyenyevu na utii kwa watu wanaokuzunguka.
"Kila jambo ni kuweka malengo,niliweka malengo, ya kupata alama tatu namkumbuka na mkuu wa shule aliniambia kwamba nitapata alama tatu nikamjibu lazima najitahidi na sasa nimeona malengo na juhudi zinasaidia zaidi na sita ishia hapa"amesema Wambura
Amesema aliposikia kwamba amepata taarifa ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita mwaka 2025 hakufikiri amefaulu bali aliwaza amefikia malengo ya alama tatu.
0 Comments