Header Ads Widget

WAKULIMA WA PAMBA KUTUNUKIWA ZAWADI KWA UZALISHAJI WA JUU

Na chausiku said 

Matukio Daima Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amewataka wadau wa sekta ya pamba kuendelea kuwaelimisha wakulima ili kuongeza tija, sambamba na kudhibiti bei ya zao hilo ili kuwapa wakulima motisha ya kuendeleza kilimo.

Hayo ameyabainisha wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa ni lazima bodi ya pamba kuendelea kuwahamasisha wakulima ili waweza kulima kilimo bora cha pamba.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda akitoa maelekezo Kwa bodi ya pamba Kuendelea kutoa elimu Kwa wakulima ili kulima kilimo bora na chenye tija 

''Kama mtawapa motisha wakulima hatua hiyo itawasaidia kuongeza uzalishaji Bora na wenye tija na kupata kipato bora"Alisema Mtandao.

Kwa upande wake, Afisa Kilimo kutoka Bodi ya Pamba, Daniel Bariyanga, alisema halmashauri zote 54 zinazolima pamba zinapaswa kuhakikisha kila mkulima anayefanya vizuri anapewa zawadi.

Afisa Kilimo kutoka Bodi ya Pamba, Daniel Bariyanga akizungumza na waandishi wa habari akiwataka wakulima wa zao la pamba kuendelea kulipa Kwa tija

“Zawadi hizi zitakuwa kwa wakulima wanaozalisha kiwango kikubwa cha pamba kwa ekari. Wanaofanikisha kilo 1,000 au 2,000 kwa ekari watatunukiwa zawadi, ikiwemo mitungi ya gesi,” alisema Bariyanga

Aliongeza kuwa Bodi ya Pamba imejiandaa kusambaza pembejeo za kutosha kuanzia mbegu, viuatilifu, vinyunyizi na mbolea hai kwa wakulima wote ili kuongeza tija katika msimu ujao wa kilimo.


Bariyanga pia aliwahimiza wakulima kujiandaa mapema kwa msimu huo ili kuhakikisha uzalishaji na unazidi kuongezeka na sekta ya pamba izidi kustawi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI