Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
WANANCHI zaidi ya 22,000 kutoka Kata za Mhunze na Kinang'weli wilayani Itilima Mkoani Simiyu wameanza kunufaika na huduma ya Maji baada ya serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kutekeleza Mradi wa Maji.
Mradi huo ambao umetekelezwa kwa gharama ya shilingi Bil.2.3 umeanza kunufaisha wakazi wa Vijiji sita vya Madilana, Mhunze, Kinang'weli, Lalangombe, Isengwa na Mwagimagi.
Akitoa taarifa ya Mradi huo, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mhandisi Hussein Yahaya amesema kuwa mradi wa Maji Kinang'weli-Madilana uliohusisha kata mbili za Mhunze na Kinang'weli ulianza kutekelezwa mwaka 2023 na umekamilika mwezi Juni 2025.
Amesema kuwa mradi huo umetekelezwa na Kampuni ya Pioneer Construction Ltd kwa gharama ya shilingi Bil. 2.3 na utahudumia wananchi 22,000 kutoka vijiji sita vya kata za Kata za Kinang'weli na Mhunze.
Ameongeza kuwa mradi huo utawapunguzia wanachi adha ya kutembea mwendo mrefu kutafuta Maji pamoja na kumaliza tatizo la kutumia Maji machafu.
"Tunampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya Maji, hadi sasa upatikanaji wa Maji katika wilaya ya Itilima umefikia asilimia 73.
Akizungumza mara ya Kuweka jiwe la msingi kwenye Mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2025, Ismail Ussi amesema kuwa serikali ya Rais Dkt. Samia amefanikiwa kutekeleza miradi ya Maji kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wanaojenga miundombinu ya Maji na kuyasambaza vijijni.
"RUWASA ndani ya nchi yentu ni miongoni mwa Taasisi zinazofanya vizuri kutekeleza miradi ya Maji,.nayasema.hayo nikiwa na ushuhuda sababu maeneoengi niliyopita wameonyesja kufanya vizuri...Miaka ya nyuma wananchi walikumbwa na tatizo la Maji, leo wananchi Wana faraja sababu Rais Dkt. Samia ametatua kero la Maji." Amesema.
Amewataka wananchi kuendelea kulinda miundombinu ya Maji safi na salama ili iweze kudumu na kuwahudumia wananchi kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa sababu serikali imeijenga kwa fedha nyingi.
Mwisho.
0 Comments