Header Ads Widget

WAGOMBEA UDIWANI KIGOMA WAKOSA WAPINZANI

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Wagombea 16 wa nafasi za udiwani wa CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa Kigoma wamefanikiwa kuwa wagombea pekee baada ya vyama vingine kushindwa kusimamisha wagombea na baadhi ya kata wagombea wa upinzani kukosa sifa.

Katibu wa uenezi,siasa na mafunzo CCM mkoa Kigoma, Deogratius Nsokolo alisema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma na kubainisha kuwa hiyo dalili njema ya ushindi katika uchaguzi huo kuelekea siku ya upigaji kura Oktoba 29 mwaka huu ambapo wagombea hao wanasubiri kupigiwq kura za ndiyo na hapana.


Nsokolo alisema kuwa katika kata hizo ambazo wagombea wa CCM wamekosa upinzani ni pamoja na wilaya ya Kasulu ikiwa na wagombea sita waliokosa wapinzani, wilaya ya Buhigwe kata tano, Kibondo wilaya ya Kibondo  ikiwa na kata nne, na wilaya Uvinza ikiwa na kata moja ya Basanza.

Akizungumzia mchakato wa kampeni za wagombea ubunge,udiwani na  za Urais za mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan alisema kuwa kampeni zitaendelea baada ya uzinduzi wa Chama hicho uliofanywa viwanja vya Kawe jijini Dar es Salaam na kwamba Mgombea wao wa urais wa chama hicho atafanya mikutano ya  kampeni  mkoani humo Septema 13 mwaka huu

Kwa upande Mgombea ubunge wa jimbo la Kasulu Mjini, Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa baada ya uzinduzi wa kampeni za chama hicho uliofanyika viwanja vya Kawe jijini Dar es Salaam anatarajia kuzindua kampeni za majukwaani Septemba nne na kwamba michakato mingine ya kampeni itaendelea kabla ya kuanza kwa mikutano hiyo ya hadhara.

Profesa Ndalichako alisema kuwa miaka mitano ambayo amekuwa mbunge kwenye jimbo hilo kulikuwa na changamoto kubwa ya barabara za jimbo hilo na kwamba tayari kwa sasa barabarani nyingine zimeanza kuchongwa sambamba na utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji ambao unaendelea kutekelezwa ambao utaondoa changanoto kubwa ya maji inayowakabili wananchi wa jimbo hilo.

Naye Mgombea ubunge wa jimbo la Buhigwe, Profesa Pius Yanda alisema kuwa baada ya uzinduzi wa kampeni uliofanywa na Mgombea uraisi wa chama hicho Agosti 28 mwaka huu sasa watafanya kampeni bila kulala kuhakikisha ushindi wa wagombea wa chama hicho mwezi Oktoba mwaka huu.

Profesa Yanda alisema kuwa wakati anapambana kupata ridhaa ya wananchi kuongoza jimbo hilo jambo la kwanza ambalo atalishughulikia akipata nafasi hiyo ni barabara ndani ya jimbo ambazo zitaunganisha barabara kuu ili ziweze kutafsiri kwa matendo uboreshaji wa miundo mbinu kuwezesha wakulima kuwa na barabara bora kwa usafirishaji wa mazao yao.


 


 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI