Na Mariam Kagenda _Kagera
Mgombea Ubunge Jimbo la Ngara kupitia Chama Cha Mapinduzi Dotto Bahemu ni Mgombea pekee katika Jimbo hilo baada ya Chama Cha Ukombozi wa Umma kushindwa kurejesha fomu na vyama vingine kutochukua fomu ya kugombea katika nafasi hiyo .
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngara Bwana Constantino Msemwa wakati akizungumza na Mwandishi amesema kuwa waliochukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo hilo ni wawili ambao ni Dotto Jasson Bahemu kutoka Chama Cha Mapinduzi na Peter Ruzige kutoka Chama Cha Ukombozi wa Umma lakini mpaka wakati wa kufungwa kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu aliyerudisha ni Jasson Bahemu pekee.
Amesema kuwa Dotto Bahemu ametimiza vigezo vyote vinavyotakiwa kujazwa kwenye fomu hivyo Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi imemteua kuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Ngara .
Ameongeza kuwa Vyama vingine havikujitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Ngara isipokuwa Chama cha Mapinduzi(CCM) pamoja na Chama Cha Ukombozi wa Umma ( CHAUMA) pekee ndo vilivyojitokeza katika zoezi hilo .
0 Comments