Header Ads Widget

UJERUMANI KUSITISHA UUZAJI WA SILAHA KWA ISRAEL ZINAZOWEZA KUTUMIKA GAZA, MERZ ASEMA


 Ujerumani itasitisha uuzaji wa silaha zake kwa Israel ambazo zinaweza kutumika katika Ukanda wa Gaza, Kansela Friedrich Merz anasema kutokana na mipango ya Israel ya kuuteka mji wa Gaza.

Akizungumza muda mchache uliopita, Merz amesema serikali yake haitaidhinisha usafirishaji wowote wa zana za kijeshi kwa Israel ambazo zinaweza kutumika Gaza hadi ilani nyingine itakapotolewa.

Merz anasema ilikuwa "inazidi kuwa vigumu kuelewa" jinsi mpango wa kijeshi wa Israel ungesaidia kufikia malengo halali, akiongeza: "Katika mazingira haya, serikali ya Ujerumani haitaidhinisha mauzo yoyote ya zana za kijeshi ambazo zinaweza kutumika katika Ukanda wa Gaza hadi ilani nyingine."

Kihistoria, Ujerumani imekuwa mojawapo ya wauzaji wakubwa wa silaha kwa Israeli.

Kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (Sipri),-Taasisi ya utafiti ambayo inaangalia migogoro na silaha, Marekani ilikuwa muagizaji mkuu wa silaha za Israel na zana za kijeshi kijeshi katika kipindi cha kati ya 2020-2024, na Ujerumani ikiwa ya pili.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI