Header Ads Widget

MTENDAJI MKUU WMA ATEMBELEA MAONESHO YA NANENANE DODOMA*


Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Alban Kihulla, leo Agosti 8, 2025 ametembelea Maonesho ya NaneNane kitaifa, uwanja wa Nzuguni jijini Dodoma.

Akiwa katika Banda la WMA, Afisa Mtendaji Mkuu amewapongeza watumishi wa Wakala kwa kazi nzuri ya kuelimisha umma ambayo wamekuwa wakiifanya tangu kuanza kwa Maonesho hayo.

Amewataka kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa jamii hata baada ya Maonesho ili wananchi waelewe ni kwa namna gani Serikali kupitia WMA inawalinda kwa kuhakikisha vipimo vinavyotumika katika sekta mbalimbali ni sahihi na vinatumika kwa usahihi. 

"Tuendelee kutumia majukwaa mbalimbali kutoa elimu ya vipimo kwa wananchi ili waelewe haki yao ya kupata huduma kwa vipimo sahihi lakini pia na wajibu wao wa kuhakikisha wanatumia vipimo sahihi katika sekta mbalimbali. "

Kihulla ametembelea mabanda mengine mbalimbali likiwemo banda la Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Taasisi zake ili kujionea huduma zinazotolewa.






 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI