……Nyabundege aweka wazi mabilioni yaliyotolewa na Rais Samia miana minne
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
RAIS Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa kazi nzuri iliyofanywa na benki hiyo katika kuleta mageuzi makubwa kwenye Sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
Alitoa pongezi hizo jana wakati alipotembelea banda hilo kwenye kilele cha amaonyesho ya wakulima nanenane yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni Dodoma.
Alisema ndani ya muda mfupi TADB imekuwa msaada mkubwa kwa wakulima ambapo waliwapa mikopo iliyowawezesha kulima kisasa na kuongeza tija kwenye kilimo chao.
TADB kama Mdhamini Mkuu wa maonesho ya Nanenane amekuwa kuvutio kikubwa kwa wananchi waliotembelea maonesho hayo kupitia elimu iliyokuwa inatolewa kwa njia ya madarasa, shuhuda za wanufaika, machapisho pamoja na maelezo ya moja kwa moja.
TADB,inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuleta mapinduzi ya kilimo kwa vitendo kupitia elimu ya kifedha, mikopo ya kimkakati, na uwezeshaji wa wakulima wadogo na wa kati. Ameyasema Hayo mbele ya ya Mhe. Rais.
0 Comments