Header Ads Widget

TRA YAELEZA MAFANIKIO MABORESHO SHERIA YA FEDHA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MAMLAKA ya mapato nchini (TRA) imesema kuwa mabadiliko ya sheria ya fedha yanayofanyika kila mwaka yanalenga kuongeza ari ya ulipaji kodi kwa hiari sambamba na kuchochea uwekezaji wa ndani ili kupunguza uingizaji wa bidhaa na malighafi kutoka nje.mekuwa na mchango mkubwa katika kuifanya mamlaka hiyo kuongeza ukusanyaji mapato na wakati mwingine kuwezesha kuvuka lengo.
 

Hayo yameelezwa na Afisa Msimamizi Mkuu wa kodi TRA,Hamad Mterry  katika semina ya siku moja kwa wafanyabiashara, wakuu wa mamlaka za serikali mkoa Kigoma na wadau mbalimbali wa biashara mkoa Kigoma kutoa elimu ya mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2025.
Afisa Msimamizi Mkuu wa kodi TRA,Hamad Mterry
        
Materry alisema kuwa Msimamizi huyo alisema kuwa mabadiliko ya sheria ya fedha ya kila mwaka hufanywa na bunge la mwisho la  mwaka wa fedha  ili  kufanyia marekebisho changamoto zilizojitokeza kwa mwaka ulioisha ambazo zilichangia kutokusanywa kwa baadhi ya mapato kwa mwaka huo lakini kuziba mianya ya ukusanyaji inayojitokeza.

Afisa huyo wa TRA alisema kuwa katika baadhi ya vyanzo vipo sababu zinazofanya wafanyabiashara na mamlaka za serikali zinazokusanya mapato kwa kuuza huduma na bidhaa  ambazo sheria zimekuwa na mapungufu kidogo katika usimamizi wake hivyo marekebisho yanayofanyika yanalenga kuweka mizani sawa katika ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye vyanzo hivyo.
viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoa Kigoma na wafanyabiashara wa mkoa huo wakiwa katika semina kuhusu mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2025 iliyokuwa ikitolewa na uongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA)

Mmoja wa washiriki wa Mkutano huo, Celestine Nestory kutoka chemba ya wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo (TCCIA) mkoa Kigoma alisema kuwa amepata manufaa makubwa ya mkutano huo kulingana na maelezo ya sheria ya mabadiliko ya fedha yaliyofanyika.
 
Alitoa mfano wa uingizaji wa bidhaa kutoka nje ikiwemo Shairi kwa ajili ya kutengeneza bia ambazo zimeongezwa kodi na kuwabana wazalishaji ambapo ameridhika na maelezo kuwa hiyo inalenga kuimarisha uwekezaji wa ndani kwenye kilimo na viwanda.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI