Header Ads Widget

TIRA NA CRDB KUNEEMESHA SEKTA YA KILIMO


Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na Benki ya CRDB zakubaliana kukamilisha uandaaji wa Kanuni za Bima ya Kilimo pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wanaohusika katika kuendesha bima hizo nchini ili kuleta neema na mustakabali mzuri wa sekta ya kilimo. 

Hayo yameafikiwa Agosti 11, 2025 kwenye Kikao maalumu baina ya Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bwn. Abdulmajid Nsekela kilichofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa Mazungumzo hayo Dkt. Baghayo Saqware amesema, Kutokana na hati ya ushirikiano (MoU) iliyosainiwa mwaka 2024 baina ya TIRA na CRDB kuhusu kufanya maboresho kwenye sera ya kilimo hakuna budi sasa kuanza utekelezaji wake kwakuwa MoU imebainisha wazi maeneo ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili hivyo CRDB kuendelea kuwezesha mchakato.

Nae kwa upande wake Bwn. Abdulmajid Nsekela amesema, Benki ya CRDB ipo tayari kuendelea kutekeleza makubaliano ili kuleta tija kwenye kilimo na kwamba inatazamia kuwa na mchakato wa uwezeshaji katika uboreshaji wa Sera ya Kilimo ambao ni shirikishi.

Maeneo mahsusi yaliyobainishwa kwenye MoU hiyo ni pamoja na mageuzi ya sera, utengenezaji wa bidhaa za bima na kujengeana uwezo.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI