Header Ads Widget

SAMIA ACHUKUA FOMU NDANI YA DAKIKA 28 INEC

Na Hamida Ramadhan, MatukioDaima Media Dodoma

MGOMBEA  wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt,Samia Suluhu Hassan, pamoja na mgombea mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo wamechukua fomu za kugombea nafasi ya urais na umakamu wa rais katika ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) zoezi lilotumia dakika 28.

Dkt, Samia aliwasili katika ofisi hizo saa 11:15 asubuhi na kupokelewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mizengo Pinda pamoja na viongozi wa juu ya CCM ambapo  zoezi la uchukuaji wa fomu lilichukua takribani dakika 28 hadi kukamilika. 

Baada ya kuchukua fomu, Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, na mgombea mwenza wake walitoka nje ya ofisi za Tume na kuwaonesha waandishi wa habari mkoba uliokuwa na fomu hizo, huku wakipiga picha na baadhi ya viongozi wa CCM waliomsindikiza.

Wakiwa na bashasha, waliondoka eneo hilo saa 11:43 asubuhi , huku Samia akiwapungia mkono baadhi ya viongozi wa chama waliokuwepo.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI