Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Caspar Mmuya, amechukua rasmi fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Ruangwa katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi zilizopo huko Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Tukio hilo limefanyika Leo 26,08,205 Katika ofisi ya tume ya Uchaguzi huko Wilayani Ruangwa ambapo msimamizi wa Uchaguzi Jimbo Hilo la Ruangwa mwalimu George Mbesigwe alimkabidhi Fomu hizo
Hatua hiyo imeashiria nia yake ya kuingia kwenye siasa za uwakilishi baada ya utumishi wa muda mrefu serikalini ambapo akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo Mmuya ameahidi kutekeleza Mpango iliyoanzishwa na Mtangulizi wake
Mmuya, ambaye anatajwa kuwa na rekodi ya utendaji mzuri akiwa mtumishi wa umma, sasa anataka kuendeleza kazi hiyo kwa kulitumikia Bunge kupitia Jimbo la Ruangwa.
Jimbo hilo Ruangwa lilikuwa likiwakilishwa na Waziri Mkuu aliyemaliza muda wake, Kassim Majaliwa, ambaye hajatangaza nia ya kugombea tena.
Hatua hii imezua hamasa kubwa miongoni mwa wakazi wa Ruangwa, wakisubiri kwa hamu kuona nani ataibuka kidedea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu
0 Comments