Ridhiwani kikwete, Mbunge wa Chalinze amechukua fomu kuomba ridhaa ya kugombea tena Ubunge wa Chalinze akiwaahidi kuendelea kupambana kwa nguvu zaidi kuleta maendeleo kwa spidi zaidi.
Akizungumza wakati akishukuru wananchi waliojitokeza kumsindikiza, Ridhiwani Kikwete alituchukua nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi wa Chalinze umuhimu wa kurudisha shukrani kwa Mh. Rais Samia kwa mchango mkubwa wa maendeleo uliofanyika.
Katika mkutano huo, ambao ulioudhuriwa na wananchi wengi, unatengeneza alama nyengine inayoonyesha matarajio makubwa katika uchaguzi ujao ambao CCM inataraji kupata ushindi mkubwa katika jimbo hilo.
0 Comments