Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yametakiwa kuwa mawakala wa mabadiliko chanya katika jamii katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye jamii.
Hayo yamesemwa leo Agosti 12, 2025 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt John Jingu wakati anazungumza katika Kongamano la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali linaloendelea kwa siku ya pili katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Dkt. Jingu amesema Mashirika hayo yanawajibu wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kifikra na maendeleo katika jamii kupita utekelezaji wa miradi yao mbalimbali.
“Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali, yamesajiliwa kisheria kwa lengo la kutoa huduma na elimu katika nyanja tofauti kwa jamii hivyo mtambue kwamba ajenda ya maendeleo endelevu katika Taifa ni pamoja na kuwa mawakala wa mabadiliko chanya katika jamii” amesema Dkt Jungu.
Aidha ameeleza kwamba Mashirika hayo yanapaswa kutekeleza miradi ya uzalishaji ambayo ni endelevu na kuondoa utegemezi kutoka kwa wafadhili, kwa sababu kwa sasa Sera za nchi za Ulaya na Marekani zimebadilika.
Ameongeza kwamba Mashirika yanapaswa kujitafakari vizuri ili kuhakikisha yanakuwa njia mbadala kuendeleza huduma na miradi kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika maeneo yao.
0 Comments