Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima Media Dodoma
NAIBU Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, ameagiza wananchi waliopisha mradi wa Umeme Kagera walipwe fidia haraka
Amesema shilingi Bilioni 2.6 zimetolewa hivyo mwezi wa 9 mwaka huu wananchi hao walipwe ili waweze kupisha kujiendeleza
Agizo hilo amelitoa leo jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini mikataba ya mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kwa msongo wa kilovoti 220 kutoka Benako hadi Kyaka, pamoja na kituo cha kupoza umeme cha Beneko chenye msongo wa kilovoti 220/33.
Aidha, maeeleza kuwa endapo hazina haijatoa pesa, Shirika la Tanesco lianze mchakato w kuwalipa wananchi wa Kagera waliopisha mradi wa umeme
" Shughuri hii Rais Samia naifahamu na amenielekeza kwamba jambo hilo lifanyike mahususi, lisifanywe kwa kificho bali kwa uwazi," Amesema.
Amesema kuwa Serikali imeamua kwa dhati kazi hiyo kufanyika Kagera na baada ya muda itakuwa chanzo kikubwa cha umeme.
"Sasa mkataba wa kuuziana umeme na nchi ya Uganda unkwenda kuisha, tuliomba kuongezewa miaka miwili, na muda utakapoisha, Kagera haitakuwa na shida ya umeme tena, " Amesema
Na kuongeza "Baada ya miaka michache, Mkoa wa Kagera hautakuwa na changamoto ya umeme, hali inayotokana na juhudi kubwa za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan," Amesema.
Dkt. Biteko amesema kuwa upatikanaji wa nishati hiyo ni maendeleo kwa wananchi na viwanda, kwani Mkoa wa Kagera umekuwa na viwanda vingi, hivyo Wanakagera watautumia umeme huo kujiletea maendeleo.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba, amesema tukio hilo ni la kihistoria kwa kuwa kusainiwa kwa mikataba hiyo kunamaanisha kuwa mikoa yote iliyokuwa nje ya gridi ya taifa sasa inakuwa na mpango wa kuunganishwa.
Amesisitiza kuwa, “Tunapotangaza kuwa vijiji vyote vya Tanzania vimepata umeme, ni hatua kubwa iliyofikiwa, " Amesema
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Razalo Twange, amesema lengo la tukio hilo lilikuwa ni kusaini mikataba miwili, hatua ambayo ni ya kihistoria na safari ndefu kwa TANESCO.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajati Fatma Mwasa, ameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa miradi hiyo kutekelezwa kwa manufaa ya Wanakagera.
Amesema kuwa Mkoa unatumia megawati 46, na kwamba kupitia miradi hiyo, mkoa utaunganishwa na gridi ya taifa, ambapo awali ni wilaya tatu pekee ndizo zilizokuwa kwenye gridi hiyo.
“Wanakwenda kuwa na umeme wa uhakika na viwanda vitafanya kazi kwa uhakika kwa kile wanachohitaji. Wanakagera tumeipokea miradi hiyo kwa mikono yote, kwani mkoa unakwenda kuongeza maendeleo zaidi,” alisema Hajati Mwasa.
Hata hivyo wafadhili wametoa Dola za Kimarekani milioni 105 kwa ajili ya mradi huo ambao utatekelezwa kwa muda wa miezi michache miezi 24 hali itakayowaondolea wakazi wa Kagera changamoto ya umeme.
Mwisho
0 Comments