Na Mwandishi wetu, Matukio Daima.
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu Mkoani Simiyu ambaye amemaliza muda wake, Luhaga Joelson Mpina kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametimkia Chama Cha ACT Wazalendo baada ya jina lake kukatwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tena nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo.
Mpina amepokelewa na viongozi wa Chama hicho akiwemo, Zito Kabwe na Katibu Mkuu Ado Shaibu katika ofisi za Chama hicho zilizopo Vuga Visiwani Zanzibar, leo August 5, 2025.
Itakumbuwa kuwa, hivi karibuni Mpina alichukua fomu ya kuomba kupigiwa kura za maoni ndani ya CCM ili aendelee kuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa lakini jina lake halikuweza kurudishwa.
Mwisho.
0 Comments