Na Matukio Daima Media.
KALENGA.
Mgombea Mteule Udiwani Kata ya Kalenga iliyopo Wilaya ya Iringa, Mkoani Iringa Shakira Kiwanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Agosti,25, 2025 amerejesha fomu rasmi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Shakira amerejesha fomu hiyo katika ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kalenga na kishakuzungumza na umati wa wana CCM waliomsindikiza kujiandaa na kampeni za nguvu katika kusaka kura za Udiwani, Ubunge, na Urais pindi muda wa kampeni utakapo wadia.
"Kwa sasa tukajiandae na maandalizi ya kampeni zitakazoanza rasmi Agosti 28, mwaka huu kwa ajili ya Udiwani, na kumuenzi kwa kura za ushindi wa kishindo Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini," amesema
Akizungumza Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi alisema kuwa kwa sasa wanalojukumu la kumnadi mmgombea mmoja tu katika kata hiyo.
“Niwashukuru wagombea wote waliojitokeza kutia nia kwa kuwa wagombea wote walikuwa sahihi na walikuwa na sifa za kugombea,lakini kutokana na ufinyu wa nafasi hivyo anayetuwakisha ni mmoja na tuungane kumpa sapoti wakati wa kampeni”alisema
Alisema kuwa ni heshima kubwa kumpa nafasi mwanamke kuipeperusha bendera katika kata hiyo na kuhakikisha wanampa kura za ndio nyingi.
MWISHO.
0 Comments