ALIYEKUWA Mjumbe wa Mkutano Mkuu CHADEMA kutoka Wilaya ya Bukene na Mgombea Ubunge jimbo la Bukene 2020, Lumola Steven Kahumbi amekihama Chama hicho na kujiunga na CHAUMMA.
Lumola ambaye ni ndugu wa Mwanasiasa maarufu wa CCM na aliyekuwa Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Khamisi Kigwangalla, amejiunga rasmi CHAUMMA hii leo Agosti 11, 2025.
Itakumbukwa hivi karibuni Lumola aliongea na Vyombo vya habari juu ya hali ya mambo yanayoendelea ndani ya CHADEMA ikiwemo hali ya msuguano.
0 Comments