Header Ads Widget

MAREKANI YAMZUIA KIONGOZI WA PALESTINA KUHUDHURIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA MJINI NEWYORK

 

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas alikuwa akipanga kusafiri kwenda New York kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amezuiwa kuhudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York mwezi ujao baada ya yeye na maafisa wengine 80 wa Palestina kufutiwa viza zao, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio aliwalaumu kwa kuhujumu juhudi za amani na kutafuta "kutambuliwa kwa upande mmoja kwa taifa la Palestina la kudhaniwa".

Uamuzi huo ambao umekaribishwa na Israel si wa kawaida kwani Marekani inatarajiwa kurahisisha usafiri kwa maafisa wa nchi zote zinazotaka kutembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Marufuku hiyo inajiri wakati Ufaransa ikiongoza juhudi za kimataifa za kulitambua taifa la Palestina katika kikao hicho - hatua ambayo utawala wa Donald Trump umeipinga.

Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa, Riyad Mansour, alisema hapo awali kwamba kama mkuu wa ujumbe wake, Abbas atahudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali huko New York.

Lakini afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje baadaye alisema Abbas na Wapalestina wengine wapatao 80 wataathiriwa na uamuzi wa kukataa na kufuta viza kutoka kwa wanachama wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) na Mamlaka ya Palestina (PA).

Ofisi ya Abbas ilisema ilishangazwa na uamuzi huo wa kumnyima viza, ambao "unapingana waziwazi na sheria za kimataifa na Mkataba wa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, hasa kwa vile Taifa la Palestina ni mwanachama waangalizi wa Umoja wa Mataifa". Iliitaka Marekani kubadili hatua hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI