Header Ads Widget

KIZA MAYEYE,SERUKAMBA MCHUANO MKALI UBUNGE KIGOMA

 

Mgombea ubunge wa Chama Cha ACT Wazalendo Kiza Mayeye  (kushoto) akipokea  fomu ya kugombea ubunge kutoka kwa Msimamizi wa uchaguzi wa tume huru ya Taifa ya uchaguzi  jimbo la Kigoma Kaskazini Linus Sikainda (kulia)  ili kugombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma.

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mgombea ubunge wa Chama Cha ACT Wazalendo Kiza Mayeye  amechukua fomu kutoka tume huru ya Taifa ya uchaguzi (INEC) ili kugombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini ikiwa ni muendelezo wa uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani unaotarajia kufanyika kwenye Oktoba mwaka huu.

Mayeye achukua fomu kutoka kwa Msimamizi wa uchaguzi wa INEC katika jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma, Linus Sikainda huku akieleza kuwa ameamua kuchukua fomu kugombea ubunge katika jimbo hilo ili kuwa sauti ya wananchi wa jimbo hilo katika kusimamia mahitaji muhimu ya kibinadamu ya wananchi hao.

Mgombea huyo alisema kuwa miongoni mwa mambo ambayo atayapa kipaumbele akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo ni pamoja na kuitaka serikali kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya sambamba na uwepo wa bima ya afya kwa wote na  upatikanaji wa huduma bora ya elimu ambayo itakuwa miongoni mwa masuala atakayopigania ikiwemo kuhakikisha serikali inaajiri walimu wa kutosha badala ya wazazi kutoa fedha kwa ajili ya kuajili walimu wa kujitolea.

Peter Serukamba mgombea ubunge jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma kwa tiketi ya CCM

 Pamoja na Mayeye pia Mgombea kwa tiketi ya CCM, Peter Serukamba naye amechua fomu ya kugombea  kutoka kwa msimamizi wa jimbo hilo la uchaguzi la Kigoma Kaskazini ambapo mgombea huyo akiambatana na wadhamini wake wachache bila kuwa na mbwembwe alichukua fomu ili kuanza mchakato wa kugombea katika jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchakato huo Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma ,Linus Sikainda alisema kuwa hadi kufikia  mchana Julai 25 mwaka huu  jumla ya wagombea ubunge kutoka vyama 11 walikuwa wamechukua fomu katika jimbo hilo.

Msimamizi wa uchaguzi wa tume huru ya Taifa ya (INEC) uchaguzi  jimbo la Kigoma Kaskazini Linus Sikainda

Sikainda alisema kuwa wagombea ambao walikuwa wamechukua fomu kugombea ubunge katika jimbo hilo ni  kutoka vya Act Wazalendo, CCM, CUF, ADA TADEA,  UDP,TLP,AAFP, ,DP,ADC, NLD na NRA ambapo zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litafungwa Agosti 27 na kampeni zitaanza Agosti 28.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI